Somo la 2
Unapoandaa na kuelewa maana ya kupima uzito, ni vema kwanza ukitumia vipimo visivyo rasmi. Kama wanafunzi watakadiria na kulinganisha uzito kwa kutumi vipimo visivyo sanifu kama vile uzito wa punje ya maharage na kizibo cha chupa wataelewa haraka kuwa hili ni upuuzi, uzito mara zote hutofautiana.
Pale wanafunzi wakijua umuhimu wa vipimo rasmi, ufundishaji wa vipimo sanifu kama gramu na kilogramu utaeleweka vema.
Uchunguzi kifani ya 2: Kutumia vipimo sanifu kupima
Chinwe, mwalimu wa shule ya msingi, alijisikia kuwa baada ya kuwafundisha wanafunzi wake jinsi ya kutumia mizani rahisi kulinganisha uzito wa vitu, sasa walinganishe vitu hivyo na ule wa vipimio vilivyochaguliwa.
Alikusanya vitu mbalimbali na kuchagua maharage kama kipimio chake. Akiwa na darasa zima wakitumia mizani, aliwaambia wanafunzi wawili waweke kitu katika kisahani kimoja na kuweka maharage mengi upande mwingine mpaka ilipokaa sawa. Walihesabu maharage kwa kila kitu kilichopimwa na kuandika idadi.
Baadaye, alitumia maharage marefu kupimia vitu vile vile na kuandika matokeo. Aliongea na wanafunzi jinsi maharage haya yanavyotofautiana idadi katika kupimia uzito wa vitu na pia aliongelea jinsi utofautishaji wa uzito ulivyo mgumu kama huyu atatumia kitu hiki na mwingine akatumia kingine.
Aliwaambia nini watafanya kipindi kitakachofuata.
Shughuli ya 2: Uwasilishaji wa Data
Kabla ya kufanya shughuli hii, soma Nyenzo rejea 3: Maelezo kwa wanafunzi katika shughuli ya kupima na kusanya vitu vifuatavyo (vya kutosha ukubwa wa darasa):
Mizani rahisi;
Vitu vyenye uzito sawa ili kutumika kama vipimio (mfano. Vizibo vya chupa na mbegu za maharage);
Vitu vya uzito tofauti (mfano. Makopo au mawe). Unaweza kukusanya vya kutosha kundi moja na makundi yakafanya kwa zamu huku wakifanya kazi zingine.
Andika maelezo ubaoni na eleza nini wanatakiwa kufanya (angalia Nyenzo rejea Muhimu: Kazi za Makundi darasani kwa ajili ya kupanga makundi darasani).
Mwishowe, waulize wanafunzi tofauti kati ya kupima kwa kutumia mbegu au vizibo vya chupa, kuliko kulinganisha tu. Nakili majibu yao ubaoni. Waulize kama hii ni namna nzuri ya kupima.
Waambie wanafunzi kuorodhesha vitu katika mtiririko kuanzia kizito zaidi kuelekea chepesi zaidi –je hili ni rahisi au ngumu kuliko mwanzo? Kwa nini?
Somo la 1