Nyenzo ya 1:
Sampuli ya Maswali
Usuli / uelewa wa mwalimu
- Unaelewa nini kuwa maana ya neno 'urefu wa mtu'?
- Utajipimaje wewe mwenyewe?
- Je wakati unapima, uvae viatu au usivae?
- Je ulale chini au usimame ukiegemea ukuta?
- Vipi kuhusu wale wenye nywele ndefu, je wazikunje?
- Upime kutoka wapi?
- Upime na kitu gani?
- Uwe sahihi kiasi gani?
- Vipi unaweza kutumia rula ya mstari au tepu ya kupimia?
- Vipi utakusanya vipimo?
Somo la 3. Kutathmini ufahamu wa urefu