Nyenzo-rejea ya 2: Mfuma ikolojia wa mahali hapo
Nyenzo ya Mwalimu kwa kupanga au kubadili nyenzo ili zitumike na wanafunzi.
Mfumo ikolojia ambao wewe na wanafunzi wako mngependa kuufikiria ungeweza kuwa na yafuatayo:
- Maisha chini ya mwamba mdogo au gogo la mti ulioanguka;
- Mti ulio jirani;
- ua;
- darasa lenyewe ( kona, kabati,n.k);
- mto au ziwa la mahali hapo;
- msitu ulio karibu;
- kilima kisicho na miti;
- furushi la miti nyumbani (angalia nyoka);
- kichaka cha miti;
- ufukwe;
- shimo la mboji.
Tunza kumbukumbu ya wanafunzi wanachotegemea kuona katika mfumo ilkolojia wao kwenye jedwali, kwa mfano ufuatao:
Chini ya mwamba
Spishi | Makadirio ya idadi | Anakula | Analiw a na | Mayai au? | Shughuli | Thamani |
---|---|---|---|---|---|---|
mchwa | Kundi zima | ant lion | Mayai mengi na lava na pupa | Wafanyak azi tofauti Wanajesh i malkia | kero vitu vifu | |
nge | Mmoja tu | majongoo nyenje kombamwi ko | nyani | vichanga | Mwiba wake una sumu | |
Andika maoni ya wanafunzi kwa penseli ili yafutwe majibu yakishajazwa.
Nyenzo-rejea ya 1: Mzunguko wa chakula