Somo la 3

Kufikiri na kuwa na tabia za kisayansi huthibitishwa pale ambapo wanafunzi wanaweza kuchunguza kitu kwa vitendo.

Uchunguzi ni stadi ya msingi katika sayansi. Inakuhusisha wewe na wanafunzi wako katika:

kuamua maswali ambayo unajaribu kuyajibu;

kuamua ni vifaa gani utakavyotumia;

kuamua ni vipimo gani na ugunduzi upi utachukua;

kuamua ni jinsi gani utawasilisha matokeo yako na jinsi gani yatakupa majibu ya tatizo lako .

Uchunguzi kifani namba 3 unaonyesha jinsi mwalimu atakavyoliongoza darasa katika kuchunguza kitu kisichojulikana. Ikiwa wanafunzi watakuwa

na maarifa ya mwongozo wa mwalimu katika uchunguzi wataweza kuandaa vizuri uchunguzi wao wenyewe kwa vitu vingine. Hivyo tunakushauri zaidi kujaribu mpango wa somo uliotolewa katika Nyenzo rejea 4: Kuandaa uchunguzi na wanafunzi wako kabla ya kujaribu Shughili muhimu

katika Shughuli Muhimu utayasaidia makundi katika kupanga, kufanya na kutoa taarifa za uchunguzi wao wenyewe wa unga mweupe usiyojulikana.

Uchunguzi kifani ya 3: Mwongozo wa mwalimu kwa utafiti wa wanafunzi

Miaka michache iliyopita baadhi yetu waliendesha semina ya kisayansi makazini katika vijiji vya mkoa wa Morogoro. katika mwendelezo wa semina, somo la sayansi liliandaliwa, likajaribiwa, na likatathminiwa na likafanywa vizuri na kwa usahihi zaidi. 

Kiini cha somo kilikuwa ni mwalimu kuongoza hatua kwa hatua uchunguzi wa tabia za unga usiyojulikana (unga wa udongo wa mfinyanzi). Kwanza, mwalimu alilenga zaidi katika kuendeleza stadi za uchunguzi na mawasiliano kwa wanafunzi wake. Kisha aliuliza: ni nini kitatokea iwapo utaweka tone la maji kwenye unga? majibu ya wanafunzi yalipelekea uchunguzi zaidi, uangalizi na mawasiliano. Katika kutafakari ilikuwa dhahiri kwamba wanafunzi walifikiri na kutenda kisayansi.

Soma habari zaidi ya mpango wa somo katika Nyenzo rejea 4. Hapa utaona somo la sanaa na kazi za mikono na lugha zilizopendekezwa.

Shughuli muhimu: Kuchunguza unga mweupe usiyojulikana

Waambie wanafunzi kuwa kila kundi (wanafunzi watatu au wanne) watapata unga mweupe usiyojulikana tofauti ili wauchunguze. Wakumbushe kuhusu tabia na hatua na mchakato wa unga wa udongo wa mfinyanzi kutoka utafiti.

Waongoze wanapoandaa hatua za utafiti wao wenyewe kwa siku inayofuata. Katika maandalizi yao lazima wahusishe vifaa wanavyohitaji na hata makisio yao. Wape muda wa kushirikiana darasani na kufanya maandalizi yao kuwa mazuri zaidi.

Siku inayofuata wape kila kundi unga mweupe kama vile sukari, chumvi, sabuni ya unga, sodiamu kaboneti, unga, unga wa chakula, matunda yenye chumvi tofauti isiyojulikana lakini salama kutumia.

Wasaidie wanapofanya uchunguzi wao na kuandaa jinsi ya kutoa taarifa ya utafiti wao.

Je wanaweza kuvitambua vitu?

Je umezipimaje kazi zao? Je ni ushauri gani utakaompa mwenzako anayetaka kufanya zoezi hili ?

Ufuatiliaji wa somo la lugha unaweza kuwa usomaji wa habari kuhusu kuweka vifurushi vya vitu vilivyotumika (angalia Nyenzo-rejea 5: Kusoma )

Nyenzo-rejea ya 1: Mchezo wa kumsaka mnyama mla mzoga