Nyenzo-rejea 4: Kupanga na kuchunguzi

Maarifa ya msingi/welewa wa somo wa mwalimu

Andalio la somo

Kabla ya somo, unatakiwa kutafuta kiasi kidogo cha udongo wa mfinyanzi mkavu, uponde na kuusaga hadi uwe unga laini uliokauka. Huuhitaji kuwa nao mwingi sana ila utoshe kulipatia kila kundi kijiko kidogo cha chai.

Hatua ya kwanza: Kutafiti kwa kuchunguza, kulinganisha na kuweka kumbukumbu

Wape kila kundi dishi dogo au kifuniko kwa ajili ya kuhifadhi unga wa udongo wa mfinyanzi. Waelekeze wachunguze kwa makini kitu hicho na kuandika yale yote wanayoyaona katika lugha za kienyeji, Kiswahili au kiingereza kwenye karatasi au madaftari yao.

Tumeona kuwa si vizuri mwalimu kujihusisha na vikundi vya wanafunzi vinapoanza kufanya uchunguzi.

Kabla ya kumaliza hatua hii, uliza maswali haya ya mwongozo kuhakikisha kuwa uchunguzi umekamilika:

  • Je umegundua madiliko katika udongo huo wa mfinyanzi je una rangi gani?
  • Je unapoushika unaleta hisia gani?
  • Orodhesha vitu vingine ambavyo unavifahamu vinavyofanana na kitu hiki

Hatua ya 1b– Mawasiliano

Yaambie makundi yaeleze ugunduzi wao. ufupishe ugunduzi huo ubaoni. Hili ni nafasi ya kuwa na lugha moja. Ikiwa wanafunzi watajibu kwa lugha ya asili mnaweza kukubaliana jibu likaandikwa kwa Kiswahili au kiingereza.

Katika hatua hii unaweza kukitambua kitu kama ni unga mkavu wa udongo wa mfinyanzi

Hatua ya 2a –kubashiri na kurekodi

Katika hatua hii waalekeze wanafunzi watumie rangi mbalimbali au aina fulani ya kalamu au kalamu ya risasi.

Gawa matone ya maji au waonyeshe wanafunzi chupa ndogo ya maji. Haya ndiyo maswali tuliyoandaa kwa ajili ya hatua hii:

  • Nini kitatokea iwapo tutaongeza matone kidogo ya maji katika kitu hiki?
  • Andika kile unachobashiri kitatokea iwapo utaongeza matone kidogo ya maji kwenye unga mkavu wa udongo wa mfinyanzi.
  • Je maji yataubadilishaje udongo wa mfinyanzi?
  • Andika mabadiliko yote ambayo kundi lako linafikiria yanaweza kutokea

Kisha waache waendelee na kazi. Baada ya dakika tano lazima uwape vichocheo kidogo. Je rangi itabadilika? Mwonekano wa kitu utabadilika? Je utaionaje?

Hatua 2b – Mawasiliano

Ongeza kazi mpya ya wanafunzi ubaoni kwa kutumia rangi mbalimbali za chaki. Tumia Kiswahili kuandika na kutoa maoni juu ya majibu yao, huku panua maarifa pale palipo na umuhimu.

Hatua ya 3a Uchunguzi, utafiti na uwekaji kumbukumbu

Badilisha tena rangi za vifaa vya kuandikia vya makundi .

Sasa waambie waongeze na kuchanganya matone machache ya maji. Je ni mabadiliko gani wanayoyaona na kuyahisi? Je ubashiri wao ulikiwa sahihi? Waambie wachunguze na kuandika yale waliyoyaona.

Hatua ya 3 Mawasiliano

Kwa mara ya tatu ziandike ubaoni kazi za makundi zilizounganishwa kwa kutumia rangi ya tatu ya chaki kama inawezekana.

Hatua ya 4 – Discussion Hatua ya 4 Majadiliano

Katika hatua hii, waambie wanafunzi waongelee na kuandika juu ya ambavyo udongo wa mfinyanzi unaweza kutumika. Andika mapendekezo

yao ubaoni. Kisha waambie wafinyange nyoka mdogo kutoka katika udongo wa mfinyanzi uliopondwa pondwa na kuchanganywa na maji kwenye dishi/ mfuniko wao. Waambie waandike au kupima urefu wake kabla ya kumuacha sehemu kavu iliyo salama. Waambie waandike kile wanachofikiri kitatokea kwenye udongo wa mfinyazi siku chache zinazofuata.

Sasa unaweza kuwa na ramani ya mawazo inayoonyesha uchunguzi na ubashiri kuhusu udongo wa mfinyanzi.

Imechukuliwa kutoka: programu ya sayansi ya awali katika kazi za mtaala

Nyenzo-rejea 3: Sampuli ya kazi za wanafunzi

Nyenzo-rejea 5: Kuongoza uhifadhi