Somo la 2

Katika sehemu 1 tulichukulia tabia za maada wakati tulipozilinganisha na mgandamizo wa yabisi, kimiminika na gesi. Sasa tunachukulia tabia zingine chache zaidi kwa kuhusianisha na yabisi.

Hii ni moja ya kufikiria, kwa nini baadhi ya vitu yabisi ni vya baridi ukivigusa na vingine havina ubaridi? Fikiria kuhusu kijiko cha mbao na kijiko cha metali. Mara ya kwanza tulipovitoa mezani lazima vilikuwa katika chumba kimoja chenye joto sawa –lakini bado kijiko cha metali kikawa cha baridi zaidi.

Baadhi ya vitu vinabeba au kupitisha joto vizuri zaidi kuliko vingine. Metali ina tabia ya kuwa kipitishio kizuri cha joto. Kijiko cha metali kinapitisha joto nje ya mikono yetu na kisha tunahisi baridi. Kijiko cha mbao ni kipitishio kibaya cha joto- ni ihami nzuri ya joto.

Katika shughuli 2 wewe na wanafunzi wako mnachunguza tabia ya uyeyukaji. Ni tabia zipi zingine mnaweza kuchunguza? Upitishi wa umeme? Densiti?

Uchunguzi kifani 2 unaonesha jinsi mwalimu mwenye darasa kubwa alivyoyasaidia makundi ya wanafunzi kuchunguza kundi moja la vitu ( angalia: Nyenzo rejea Muhimu: kufanya kazi na darasa kubwa au madarasa ya ngazi mbalimbali.

Uchunguzi kifani ya 2: Tabia ya metali

Jumatatu Maria Swai alileta vitu mbalimbali vya metali kutoka nyumbani na kuvipanga kwenye meza yake iliyo mbele ya darasa. Vilihusisha pete za dhahabu, fedha ya zamani na sarafu za shaba, chuma, chuma cha pua na msumari wa shaba nyeupe na skrubu na nyaya za aina mbalimbali.

Wakati watu wengine darasani wanaendelea na kazi zingine alilipata kundi ambalo litachunguza na kutafiti tabia za metali mbele yake. Walishughulikia na kujadili nini kilichoonyeshwa. Walihoji kuhusu endapo metali ina dunda. Walianza kuuliza maswali: je metali zote zinang’aa? Ni metali gani ambayo ni ngumu na yenye nguvu zaidi? Je kufifia mng’ao na kutu ni tabia za metali?

Maria pia alipendekeza baadhi ya maswali je metali zote zinapitisha umeme? Vipi kuhusu sumaku? Aloi ni nini? Waligundua kwamba kuna tabia nyingi zinazohitaji kufanyiwa uchunguzi lakini zingine katika ngazi nyingine (angalia Nyenzo-rejea 2: kuangalia tabia za yabisi ili uweze kupata mawazo zaidi juu ya namna ya kuandaa somo kuhusu yabisi).

Aliwasaidia kwa muda wa wiki/juma wakati wakiandaa kuwasilisha matokeo ya utafiti wao. Wiki/juma linalofuata, kundi lingine litasaidiwa kufanya kazi yake katika vitu vingine kama vile plastiki au mbao.

Shughuli ya 2: Upoteaji- tabia ya uyeyushaji

Hii inajenga kazi ulizofanya na wanafunzi katika tendo la msingi la sehemu 1 ambapo wanafunzi walichunguza vitu vya unga mweupe usiojulikana.

Anza kwa kujadili nini kitatokea utakapoweka kwenye chai kitu kinacho yeyuka kama sukari. Je utasemaje kwamba kitu kimeyeyuka? Pengine kwa wanafunzi wakubwa utatumia nafasi hii kuelezea istilahi kama vile kiyeyusho (kimiminika cha chai ya moto), kiyeyuka (sukari) na myeyuko (maji/ kimiminika kitamu kinachotokea)

Wape wanafunzi vitu vitano vyenye majina na chombo cha maji. Ni vitu gani kati ya hivi vinayeyuka kwenye maji? Waambie wabashiri na kuandika matokeo ya utafiti wao katika jedwali huku wakitumia maneno kama ‘inayoyeyuka kidogo’ na inayoyeyuka bila kusita (angalia Nyenzo rejea Muhimu: kutumia uchunguzi darasani.

Mwisho, waambie kila kundi kuandaa utafiti wao wenyewe wa vitu tofauti vinavyobadilika (kitu ambacho kinaweza kubadilika) kwamba kinaweza kuathiri uyeyukaji wa sukari katika maji. Fikiria vitu kama hali ya joto ya kimiminika (kiyeyuko); ukubwa wa chembe chembe za sukari (kiyeyushwa) kikorogeo au Chombo cha kutikisa. Utakuwa unataka kupendekeza wanafunzi wafikiri jinsi ya kuwasilisha matokeo yao kama chati. ( angalia Nyenzo rejea 3: andalio la somo juu ya uyeyushaji