Nyenzo ya 2: Kuangalia sifa za vitu vigumu vilivyoshikamana

Nyenzo ya mwalimu kwa kupanga au kurekebisha ili kutumia pamoja na wanafunzi

Vitu vingi hutokana na vile vigumu vilivyoshikamana. Vitu vigumu vilivyoshikamana huja katika maumbile mbalimbali, kila kimoja na sifa zake mwenyewe. Sifa za vitu vigumu lazima ziwe zinafaa kwa ajili ya kitu ambacho kitatumiwa kutengenezea.

Shughuli moja kwa ajili ya wanafunzi wako ni kupeana mawazo kuhusu vitu vinavyoweza kuwa na sifa mbalimbali. Weka maonyesho ya vitu darasani kote. Weka alama kwa kila kitu pamoja na maswali kadhaa (angalia chini kwa ajili ya mifano). Wanafunzi wakiwa wanafanya kazi wawili wawili, watumie dakika 20 kuangalia vitu na kujibu maswali kuhusu vifaa ili kuwasaidia kuelezea sifa za vitu hivyo.

Haya hapa ni baadhi ya mawazo ya vitu na alama kwa ajili ya maonyesho yako:

KituStudio

Kipande cha waya wa shaba

Chukua waya. Je unaweza kuupinda? Wapi umeona unatumika? Nini kinaweza kupita ndani yake?

Kikapu cha kusukwa

Unakihisi vipi kikapu? Unaweza kukirarua kwa urahisi?

Kijiko cha chuma

Chukua kijiko na ufikirie maneno matatu kuelezea hisia unayoipata ukikikamata. Inatokea nini ukiweka ncha moja ya kijiko katika kikombe cha maji ya moto?

Kikombe cha udongo

Unaweza kubadili muundo wa chombo kilichofinyangwa? (USIJARIBU HII.)

Kipande cha gilasi

Je unaweza kuona kwa kupitia kuta za gilasi? Inatokea nini ukikidondosha? (USIJARIBU HII.)

Mfuko wa plastiki

Inatokea nini pindi ukidondosha maji juu ya mfuko wa plastiki? Je yanapita ndani ya mfuko? Unaweza kuukunja mfuko kwa urahisi?

Kijiko cha mbao au mwiko

Unaweza kukipinda kijiko? Inatokea nini ukiweka ncha moja ya kijiko katika kikombe cha maji ya moto?

Kipande cha kitambaa (cha pamba)

Weka kitambaa mbele ya uso wako. Unaweza kuona upande wa pili? Unakihisi vipi?

Sumaku ndogo na pini

Itembeze sumaku juu ya pini. Inatokea nini? Umeona wapi sumaku inatumika?

Wakati wanafunzi wako wakiangalia vitu, unapaswa kuzunguka darasani huku ukizungumza na wanafunzi kuhusu nini wanachunguza. Mwishoni mwa kipindi, wakusanye wanafunzi wako na waulize wanafunzi mbalimbali wakuambie nini walichochunguza kuhusu kimoja cha vitu walivyoviona. Jenga orodha ya sifa kwenye ubao wako au ukuta darasani. Kama wanafunzi wako hawana uzoefu wa maneno haya ya sifa kwa lugha ya Kiingereza, waache watumie lugha yao wenyewe. Unaweza kuweka maneno ya Kiingereza katika sehemu inayoonekana darasani ili kuwasaidia wanafunzi kujifunza maneno haya.

Hii ni orodha ya mfano:

ImaraInsuleta (joto na umeme)
GumuHaipasuki
GumuYenye nguvu za sumaku
Isiyo pindikaKondakta ya kupitisha (joto na umeme)
Inaweza kupindikaRahisi kukata
Inayoonekana waziGhali/rahisi: Gharama
Isiyoonekana waziIsiyo nyororo/Nyororo
Joto la kuyeyusha (la juu/la chini)Isiyopenya maji

Hakikisha kwamba wanafunzi wako wanaweza kueleza maana ya kila sifa na waambie wachore jedwali katika vitabu vyao kuonyesha kila sifa na kuweka mfano wa kifaa chenye sifa hiyo m.f.

SifaIna maana ganiMfano
InsuletaHairuhusu joto kupenya Mbao

Sasa wape wanafunzi wako maswali yanayohusu kuchagua vifaa. Hii hapa baadhi ya mifano:

  • A.Isanga anapanda mboga karibu na nyumbani kwake lakini anahitaji njia ya kulinda mimea yake michanga kutokana na ndege. Ni aina gani ya muundo angejenga? Vifaa gani anapaswa kutumia? Kwa nini achague vifaa hivi?

  • B.Gagwala anataka kuweka bao jipya juu ya meza yake ya jikoni; Ile ya zamani imejipindapinda na imejaa alama za kuungua. Ni aina gani ya kifaa atumie kwa meza yake mpya?

  • C.Samuel anahitaji mfuko kubebea vitabu vyake shuleni. Achague aina gani ya kifaa kwa ajili ya mfuko huo?

Kwa kila tatizo, wanafunzi wanapaswa kufikiria kitu gani kinahitajika kufanywa, na kuchagua, kutoka katika orodha yao, sifa zinazopaswa kuwa nazo. Baada ya hapo wanaweza kuchagua kifaa kitakachokuwa bora katika kila hali.

Nyenzo ya 1: Kutengeneza kitabu cha zigizaga

Nyenzo ya 3: Mpango wa Somo juu ya uyeyukaji