Nyenzo ya 3: Mpango wa Somo juu ya uyeyukaji

Nyenzo ya mwalimu kwa kupanga au kurekebisha ili kutumia na wanafunzi

Matendo ya kuyeyuka

Hii ni njia moja ambayo unaweza kuzungumza na wanafunzi wako kuhusu wazo la kuyeyuka.

Fikiria kitu kitamu kama peremende kali au tunda tamu lililochemshwa. Unaiweka ndani ya mdomo wako na kufurahia ladha ya utamu au ladha ya tunda. Lakini haitoishi milele. Inapungua na kuwa ndogo na hatimaye inapotea yote. Imeenda wapi? Katika mchanganyiko wa sukari na mate uliyokuwa ukiyameza wakati utamu upo mdomoni. Matokeo ya uyeyushaji ni mchanganyiko wa sukari na mate.

Labda ungeweza kuwa na mashindano katika darasa lako kuona akina nani wanaweza kushikilia myeyuko wa utamu katika vinywa vyao kwa muda mrefu iwezekanavyo. Je washindi walifanyaje?

Ikitafunwa tu kidogo basi na utamu unamegeka katika vipande vidogo vidogo – umepoteza! Izungushe zungushe mdomoni na utakuwa umepoteza pia! Lakini kama ukiweza kuishikilia katika hewa baridi iliyo nchani mwa ulimi wako, ambako pia kuna mate kidogo sana, unaweza kuwa mshindi

Mifano kama hii itawapatia wanafunzi wako mawazo kiasi, kuhusu mambo yanayoathiri uyeyukaji.

Kuchunguza uyeyukaji

  1. Kila kundi la wanafunzi linachagua kigezo kinachohusika na uyeyukaji ili kuchunguza. Baadhi ya mawazo ni:
    • joto la maji (jaribu moto, jotojoto, joto la chumba na ubaridi sana);
    • kubadilisha ukubwa wa vipande vya sukari (jaribu vibonge vinne: donge moja, donge moja lilovunjwa katika vipande vidogo vidogo, donge moja katika chembe chembe na donge jengine lililopondwa kuwa kama unga);
    • kukoroga (jaribu kutokoroga, kukoroga polepole na kukoroga kwa kasi).
  2. Weka maswali haya kwenye ubao ili kuwasaidia wanafunzi wako kupanga uchunguzi wao:
    • unataka kugundua nini?
    • Unatabiri kitu gani kitakachotokea?
    • Kifaa gani utahitaji?
    • Utabadili nini kila wakati?
    • Nini utaendelea kukiweka bila ya kubadili (ili kuhakikisha kwamba jaribio ni sahihi)?
    • Je utapima nini hasa?
  3. Hakikisha kwamba kila kikundi kimefananisha mambo yote mengine na yako sawa sawa (bila kubadilika). Kigezo kimoja tu ndiyo lazima kiwe tofauti kwa kila kikundi. Kwa mfano, kama wanachunguza kukoroga, lazima watumie kiasi kile kile cha maji katika joto lile lile na kiasi kile kile cha sukari kila mara.
  4. Waambie wanafunzi wako waingize matokeo yao katika fomu ya grafu kama ile ya hapo chini, ambayo inaonyesha dakika ngapi ilichukua kwa kijiko kimoja cha sukari kuyeyuka ndani ya kiwango sawa cha maji lakini kipimo cha nyuzi za joto tofauti.

Maarifa ya usuli kwa ajili ya mwalimu

Modeli ya kuyeyuka

Hii ni picha wazi zaidi ya kile kinachotokea wakati mata ngumu inapoyeyuka katika mmiminisho majimaji. Kitu kigumu cha kuyeyuka kinakumbana na mmiminiko majimaji wa kuyeyusha. Huu mmiminiko majimaji huja ‘kuziganduwa’ chembe chembe za kitu kigumu, na kuziwezesha kutembea, kuchanganyika na kupenya kwa uhuru baina ya chembe chembe za mmiminisho majimaji.

Mambo yanayoathiri muda unaochukua kwa kitu kigumu kuyeyuka ni:

  • hali ya joto la mmiminiko wa kuyeyusha (huwa haraka katika maji ya moto);
  • Ukubwa wa kimumu au chembechembe za kuyeyuka (huwa kwa kasi kama ni chembe chembe ndogo);
  • harakati za mmiminiko wa kuyeyusha (kukoroga hufanya kuyeyuka kuwa haraka).

Mfano – kuyeyuka kwa chumvi

Kijiko cha chumvi ni chembechembe za kuyeyuka. Maji ndani ya gudulia ni mmiminiko wa kuyeyusha. Mara tu chumvi inapotumbukizwa ndani ya mmiminiko wa kuyeyusha, mchakato huitwa kuyeyuka. Matokeo ya mchanganyiko huu ni myeyusho wa chumvi na maji (chumvi chumvi).

Kama chumvi zaidi itaongezwa hadi pale itakapokuwa haiwezi tena kuyeyuka, basi tunakuwa na myeyusho ulioloa kabisa.

Nyenzo ya 2: Kuangalia sifa za vitu vigumu vilivyoshikamana

Nyenzo ya 4: Mbio za kutoweka kwa mapande ya barafu