Nyenzo ya 4: Mbio za kutoweka kwa mapande ya barafu

Nyenzo ya mwalimu kwa kupanga au kurekebisha ili kutumia na wanafunzi

Panga darasa lako katika makundi ya watoto wane wanne au watano watano.

  1. Kwa kila kikundi, chagua mtu mmoja kuwa 'mwangalizi huru'. Mwangalizi huyu atatoa taarifa kuhusu:

    • jinsi gani kikundi kilifanya kazi kwa pamoja;
    • jinsi gani kikundi kilitatua matatizo;
    • muda gani walichukua kufanya hivyo.
  2. Hii hapa ni changamoto: Kila kikundi kina mche mraba wa barafu wa ukubwa wa wastani katika mfuko wa plastiki. Tafuta njia bora zaidi ya kuifanya barafu kupotea bila kuwacha alama yoyote, hata chembe moja ya tone la doa la maji!
  3. Katika ubao, mtazamaji wa kikundi anaandika matokeo katika Jedwali kama hili hapa chini.
  4. Kila dakika, mwangalizi wa kila kikundi anaweka 'X' kama kuna hata chembe tu ya barafu iliyobaki.
  5. Kabla ya mashindano kuanza, wape wanafunzi muda wa kuongea na kupanga jinsi ya kuweza kufanya barafu kupotea

    Wakati: Dakika

12345678910Actions taken
A
B
C
D
E
F

Kikundi

  1. Kikundi gani kilipata njia ya kufanya mche mraba wa barafu yao kutoweka kwa kasi zaidi? Nani alikuwa wa pili katika njia bora? Ni kundi gani kilikuwa na mafanikio ya mwisho?
  2. Wape waangalizi nafasi ya kuripoti jinsi kila kikundi kilivyofanya kazi kwa pamoja. Wangeweza kutumia mpango wa tathmini kama huu ili kuwawekea alama za ushindi kila kikundi.
5 Nzuri sana Imetia foraKila mmoja kashiriki kikamilifu. Kila mmoja alikuwa makini, alifanya mapendekezo na kusaidia kivitendo. Kila mtu alishirikiana vizuri.
4 Nzuri sanaWatu wengi walishiriki na walikuwa na nafasi ya kufanya na kusaidia. Kila mtu alifurahia. Hakuna mtu aliyeona hakushirikishwa kitu.
3 NzuriWanakikundi walikaa pamoja na kuhakikisha kazi imefanyika. Lakini baadhi yao walikuwa kimya kidogo au hawakupata nafasi ya kusaidia.
1-2 DhaifuKikundi hicho hakikujipanga. Mtu mmoja alichukua jukumu lote. Hakukuwa na ushirikiano wa mawazo au majadiliano kuhusu nini kinatokea.

Fuatilia mbio za mche wa barafu

Jadili mabadiliko ambayo wanafunzi waliyaona wakati mche wa barafu ulipokuwa ukitoweka. Namna gani barafu ngumu hubadilika (kuyeyuka) kuwa majimaji na hatimaye kubadilika (mvuke) kuwa gesi isiyoonekana au mvuke? Haya huitwa mabadiliko ya awamu. Maliza somo kwa kufanya jaribio hili la haraka. Fanya hii chemsha bongo ya haraka:

  • Orodhesha mambo unayoweza kufanya ili kuharakisha mchakato wa kuifanya barafu imara kubadilika kuwa maji mmiminiko.
  • Neno gani la kisayansi linaelezea mabadiliko kutoka kitu kigumu hadi majimaji?
  • Orodhesha mambo ambayo yanaongeza kasi ya mchakato wa kugeuza maji mmiminiko kuwa maji ya mvuke wa gesi.
  • Neno gani tunatumia kwa ajili ya mabadiliko kutoka majimaji mmiminiko hadi gesi?

Vidokezi vya jawabu:

Mambo yanayoathiri kuyayuka na kuwa mvuke ni:

  • joto;
  • ukubwa na umbile;
  • mzunguko wa hewa;
  • shinikizo

Wanafunzi wanaweza kuandika ripoti fupi kuhusu nini wamejifunza katika mbio ya kazi za shule kwa kufanyika nyumbani

Nyenzo ya 3: Mpango wa Somo juu ya uyeyukaji

Nyenzo ya 5: Molekyuli na Atomu