Somo la 1

Kwa sababu maji ni muhimu sana katika dunia, tunasisitiza juu ya hili wakati wanafunzi wanapojifunza kuhusu vimiminika. Uchunguzi kifani 1 unaeleza ni jinsi gani mwalimu aliweka kumbukumbu ya mawazo ya wanafunzi kuhusu maji katika ramani ya mawazo ambayo aliendelea kuongezea mawazo katika mada yote.Unaeweza kutumia ramani ya mawazo kama chanzo cha mada hii? Baada ya kutengeneza ramani ya mawazo au kutumia njia nyingine kuchunguza ufahamu wa wanafunzi, maonyesho ya vitendo ni muhimu. Hii inakazia mawazo/maarifa na kuonyesha ni jinsi gani vitu vinafanya kazi au kutokea.

Katika Shughuli 1 utafanya moja kati ya maonyesho ya vitendo amabayo yanaweza kutumika kuonyesha tabia za maji.

Kwa miaka mingi sana watu walitambua nguvu za mtiririko wa maji. Kama maji yataelekezwa kutiririka chini au juu ya gurudumu inafanya gurudumu lizunguke. Hii inaweza kutumika kuendesha mashine zingine ambazo zinafanya kazi kama kusaga chakula au kufua umeme.

Kama huna maji ya kutosha kuhusiana na onyesho hili, tunakushauri kujaribu maonyesho mengine kama vile “utaonyeshaje kuwa kuna mvuke wa maji katika hewa jangwani? ( Nyenzo rejea 1: kumudu maisha jangwani inaelezea tendo hili).

Uchunguzi kifani ya 1: Kujenga taswira kubwa na kuibua maswali

Afua wa Winneba, Ghana, mara kwa mara anaanza somo jipya kwa njia murua kw a kuwaweka wanafunzi wake wa darasa la 4 pembeni mwake. Alikaa kwenye meza ndogo, na karatasi nyeupe kabisa. Alijadili mada kuhusu ‘maji’ pasipo urasmu.

Aliwauliza wanafunzi wanajua nini kuhusu maji. Aliwahamasisha wasikilizane kwa makini na kuongezea kwenye maoni ya wengine. Hakuliona wazo lolote kuwa ni kosa lakini aliwaaambia wanafunzi wafikirie kwanza kabla ya kuongeza wazo lolote katika ramani ya mawazo, na kujadii ni wapi litafaa kuwekwa.

Alihakikisha kuna mantiki kwenye ramani ya mawazo. Dora alipotaja

‘mafuriko’ wote walikubaliana kuwa maji yanaweza kuwa ni hatari, na neno hili liliandikwa kwenye mifano ya hatari. Uchafuzi wa hewa na sumu zilizoyeyushwa vilipojadiliwa haya pia yalihusishwa na hatari.

Baadaye, waliandika kwenye madaftari yao ya sayansi aliyotengeneza Afua. Wakati wakifanya hivi walifikiria juu ya mapungufu ya maarifa waliyo nayo. Maswali ya yanaongezwa kwenye ramani ya mawazo kwa kutumia rangi tofauti. (Angalia nyenzo rejea 2 Ramani raisi ya mawazo ).

Shughuli ya 1: Maelekezo/maonyesho kwa vitendo darasani- Gurudumu la maji

Maelekezo haya yanaonyesha wanafunzi kwa njia ya maigizo nguvu ya maji yanayotiririka,lakini kwa njia rahisi zaidi . Nyenzo rejea 3: maelezo ya kutengeneza gurudumu la kupandisha maji kutoka kwenye kisima inakuonesha ni jinsi gani udongo wa mfinyanzi/ plastiki iliyochomwa inayozunguka mpira inaweza kushika kadibodi kuwakilisha gurudumu rahisi la kupandisha maji. Kama tyubu ina uhuru wa kuzunguka kijiti/kifimbo na kamba iliyoloanishwa imefungwa katika hiyo

tyubu, hivyo maji yanayotiririka kuzunguka ukingo wa gurudumu yatasukuma hiyo kamba kuzunguka hiyo tyubu ya kusokotea na kunyanyua uzito.

Tunapendekeza ujaribishe hili kwanza kabla hujawaonyesha wanafunzi wako.Panga maswali utakayowauliza wanafunzi:

Ulishawahi kuona hili wapi?

Je gurudumu la kusukuma maji lina kazi gani ?

je nyenzo hii inakuwa muhimu wapi?

Unaweza kuendeleza mazoezi hayo kwa kuona kwamba kubadilisha ncha au pembe ya kisu inafanya gurudumu liende mbio .

Zoezi hili linaoanisha sayansi na teknolojia. Utakapoacha kutiririsha maji, kuna tatizo; ile kamba itajifungua. Katika teknolojia wanafunzi wanafurahia kuumba kitu kuzuia kujifungua kwa kamba au kutumia kifaa hicho kufanya kazi.

Sehemu ya 3: Kuangalia vimiminika