Somo la 2

Kuna utabiri kwamba wakati ujao vita vitapiganwa juu ya maji- wazo la kushangaza. Maji ni moja ya rasilimali muhimu sana. Je tutahakikisha vipi kwamba wanafunzi wetu wanayathamini maji na kuenzi matumizi ya maji hayo kwa uangalifu?

kiasi cha maji kinachopatikana katika ardhi ni kiasi cha lita millioni million

1,400. Maji mengi yanapatikana katika maeneo matatu:

bahari na maziwa (97%);

barafu iliyoganda kama theruji (2%);

maji yaliyoko chini ya ardhi (1%).

Pia kuna maji katika maziwa na mito, katika anga na katika viumbe hai.

Uchunguzi kifani 2 unaonyesha namna ya kuhusisha sayansi na lugha katika mazoezi ya maigizo kuhusu usambazaji wa maji. Ni muhimu kutumia mazoezi ya aina mbalimbali katika sayansi sababu kila mawanafunzi atakuwa na njia yake ya kujifunza. Wengine wanajifunza vizuri zaidi kwa matendo na wengine kwa kuona na baadhi ya wanafunzi watafurahia zaidi kusikiliza.

Katika Shughuli 2 unapanga jinsi ya kufanya majaribio ya kutenganisha maji safi kutoka katika maji ya chumvichumvi au maji machafu. Kama ilivyo katika majaribio yoyote tunashauri zoezi hili lifanyike nje ya darasa.

Ufikiri kwa makini kuhusu maswali utakayowauliza wanafunzi katika kipindi cha mazoezi.

Uchunguzi kifani ya 2: Asante kwa maji ya kunywa

Rehema Selemani anawahusisha wanafunzi wake katika kujifunza pale inapowezekana. Kwa suala la maji anaoanisha sayansi na lugha kwa kutengeneza ‘kitabu kikubwa’ na darasa lake. Anaandaa kila kitu kabla ili somo lililounganishwa liweze kwenda vizuri.

Alianza kwa kuwashirikisha wanafunzi wake na kutengeneza igizo dogo darasani. Alimwita Bakari aje mbele na akamwambia “hapa kuna kikombe cha maji ya kunywa kwa ajili yako”. Kijana aliitikia kwa unyenyekevu “Asante mwalimu kwa maji”. Kwa kushangaza mwalimu alijibu ‘usinishukuru mimi kwa ajili ya maji ya kunywa kishukuru…( alionyesha kikombe)

Kwa hiyo Bakari alikishukuru kikombe. ‘Usinishukuru mimi ‘kilisema kikombe, ‘nimebeba tu maji’ mshukuru… (‘Bomba!’ Wanafunzi wachache darasani wakasema) ‘hiyo ni kweli’ alisema Rehema na kumwambia

Yohana aje awe bomba

Hivyo Bakari alikwenda kulishukuru bomba ‘usinishukuru mimi’, lilisema bomba (Yohana), nimetiririsha maji tu. Mshukuru…’ ( mdomo wa bomba la maji! wanafunzi wengi wakasema) somo likaendelea kwa kujenga hadithi ya usambazaji wa maji vijijini/katika makazi hadi sehemu ya kuhifadhia maji, nyumba ya mashine ya kusukuma maji na kuendelea ( soma maelezo kwa undani zaidi juu ya somo hili ukizingatia ushauri katika Nyenzo rejea 4: Utengenezaji wa kitabu kikubwa).

Shughuli ya 2: Kupata maji safi

Inawezekana kutengeneza maji safi ya kunywa kutokana na maji machafu au maji yenye chumvichumvi. Waulize wanafunzi: je tutafanyaje hili? Sikiliza mawazo ya kila mmoja na uyaandike ubaoni au ukutani.

Waonyeshe wanafunzi wako namna unavyoweza kutengeneza maji machafu au ya chumvichumvi kunyweka. Chemsha kiasi cha maji kwenye chombo. Weka glasi Juu ya chombo katika pembe fulani inayoelekea katika chombo kingine cha kuhifadhia.

Maji yatakapochemka yatageuka kuwa mvuke. Mvuke utageuka kuwa kimiminika katika glasi na kuvujia kwenye chombo kingine. Elezea hatua hii kwa wanafunzi wako. Utahitaji kufanya hili mara kwa mara na kuandika istilai/maneno muhimu ubaoni.

Waambie wanafunzi kuangalia maji mapya na kuyaelezea. Nini kimebaki katika chombo cha kwanza? Mchakato huu unaitwa unekaji.

Sasa waambie wanafunzi wako wafanye kazi katika makundi kufanya ubunifu wa mipango mikubwa ya baadaye kwa ajili ya jaribio hili. Wanawezaje kupata maji safi ya kutosha kwa ajili ya familia zao. Waambie wawasilishe mawazo yao na kama darasa wajadili mapendekezo tofauti. (angalia Nyenzo rejea 1 kwa ajili ya mawazo).