Somo la 3

Kwa sehemu ya mwisho ya kazi hii tunajenga mawazo kutoka katika sehemu mbili za mwanzo kwa kuwaambia wanfunzi watatue matatizo katika shughuli muhimu (soma hili sasa). Shughuli hii inatumia staidi za uchunguzi- kubashiri, kupanga, kuweka kumbukumbu na kuwasilisha matokeo. Je aina hii ya zoezi linawafanya wanfunzi wako waendelee kuvutiwa? Unaweza kufikiria mada nyingine katika mtaala wa sayansi ambapo unaweza kuitumia njia hii? Badilishana mawazo na wenzako. Pengine unaweza kuanzisha jarida la uchunguzi katika shule yako.

Mara nyingi, katika sayansi yale yasiyotarajiwa hutokea. Katika uchunguzi kifani 3 , mwalimu mmoja alitumia maelezo kutoa changamoto kwenye fikra za wanafunzi wake - alionyesha kwamba sindano ya metali inaelea. Je hiyo inaelezewaje? Aina ya zoezi hili linakupa nafasi ya kupima uelewa wa wanafunzi na kuongezea kwenye ramani ya mawazo ya darasa ya toka mwanzo.

Uchunguzi kifani ya 3: Sindano inaelea –kuchunguza mvuto wa sura

Barnabas Haule amekuwa anafurahishwa na taharuki tangu akiwa mtoto. Katika ufundishaji wake wa sayansi anafurahia kutafuta njia zisizotegemewa kuelezea kweli zilizomo katika vitabu. Haya maelezo mafupi ghafla aliwashangaza wanafunzi wake na kuwafanya wafikirie kwa makini kuhusu asili ya maji.

Aliviweka pamoja bakuli ya kioo iliyofunuliwa, yenye maji ujazo wa robo tatu, sindano za kawaida za kushonea, mkasi na karatasi ya shashi /tishu.

Kwanza aliwaambia wanafunzi wabashiri ni nini kitatokea ikiwa utaweka sindano katika uso wa maji. Wote walitoa jibu kwa kujiamini kuwa sindano itazama. Barnabas alimwambi a mmoja wao ajaribu- ubashiri wao ulikuwa sahihi.

Baadaye, alichukua sindano nyingine na kukata mstatiri wa karatasi ya shashi kidogo ndefu kuliko sindano na yenye upana wa senti mita 2. alimenya matabaka yote mawili na kuiweka sindano kwenye moja ya mistatiri. Kwa uangalifu mkubwa aliiweka mistatiri yote kwenye maji

‘angalia inaelea’ aliliambia darasa lake. Wote walisema alikuwa anadanganya. Lakini pia kadri walivyangalia karatasi ya shashi ililowana na kuzama, likaicha sindano inaelea katika ngozi nyembamba ya uso wa maji.

Hakutoa maelezo yoyote. Aliwaambia wanfunzi wake wajadili mawazo yao na maswali katika makundi madogo madogo. Kisha akawaambia wapendekeze maelezo ya kile walichokiona na alichangia baadhi ya mawazo kuhusu mvuto wa uso

Mwishoni wa somo, baadhi ya wanafunzi hawa waliongeza taarifa mpya kwenye ramani yao ya mawazo kuhusu maji (angalia Nyenzo rejea 5: Mvuto wa uso inakupa taarifa za msingi wewe mwalimu).

Shughuli muhimu: Ni njia gani nzuri zaidi ya kukausha nguo?

Wapange wanafunzi wako katika makundi ya watu wanne. Wape kila kundi kipande cha nguo au taulo waloanishe kisha wakikate. Sasa waambie wafikiri njia nzuri ya kukausha kipande cha nguo. Je nguo itakuwa yenye makunyanzi? Iliyokunjwa? Iliyotandazwa? juani? kivulini? Penye upepo?

Kila kundi lazima lifanye ubashiri wake na kupanga jaribio lake. Watahitji vifaa gani? Watapima nini? Watawasilishaje matokeo yao?

Jadili na wanafunzi wako uhitaji wa kuweka kila kitu sawa isipokuwa kile wanachokichunguza- hapa, hii ni njia yao ya kukausha. Kwa hiyo watahitaji kuhakikisha kwamba mwazoni kila kipande cha nguo kina ukubwa sawa na kina kiwango sawa cha maji.

Wanafunzi watakapokuwa na mipango yao na vifaa vyao waache wafanye uchunguzi wao.

Kila kundi wawasilishe matokeo yao darasani; waelezee njia nzuri ya kukausha nguo na vitu ambavyo havikuenda sawa katika uchunguzi wao.

Nyenzo-rejea ya 1: Kuishi jangwani