Sehemu ya 4: Kuchunguza hewa
Swali Lengwa muhimu: Je utawezaje kutumia kifani/modeli, majaribio na majadiliano ili kuwasaidia wanafunzi kujenga picha ya hewa?
Maneno muhimu: gesi; hewa; chembechembe; upimaji; mtindo; uchunguzi
Matokeo ya ujifunzaji
Mwishoni mwa sehemu hii, utakuwa umeweza:
- kujua jinsi ya kusaidia wanafunzi kujifunza lugha katika Sayansi;
- kuchunguza mawazo kuhusu hewa na chembechembe na wanafunzi;
- kutumia njia mbalimbali za kupima wanafunzi wako.
Utangulizi
Sehemu hii ina malengo makuu mawili:
kuongeza ufahamu wako binafsi wa jinsi gani lugha itawasaidia wanafunzi kadri wanavyofikiri na kuwa na tabia za kisayansi;
kufanya hivi unawasaidia wanafunzi kufahamu asili na tabia za hewa.
Nyenzo-rejea 5: Mvuto wa uso – taarifa kwa walimu