Sehemu ya 5: Hekima katika matumizi na urejelezaji wa matumizi ya maunzi/rasilimali (vitu, vifaa)

Swali Lengwa muhimu: Je unawezaje kukuza mwelekeo sahihi wa kutumia na kurejelea matumizi ya maunzi/rasilimali ?

Maneno muhimu: inayoweza kutumika; urejelezaji; mboji; miradi; kutathmini; amali.

Matokeo ya ujifunzaji

Mwishoni mwa sehemu hii, utakuwa umeweza:

  • Kutumia njia mbalimbali kukuza mwelekeo/mtazamo sahihi wa matumizi na urejelezaji wa matumizi ya maunzi;
  • Pangilia kazi maalum za matumizi na urejelezaji wa matumizi ya maunzi/rasilimali;
  • Fanya kazi na wanafunzi wako kujenga vigezo vya kutathmini matokeo na michakato.

Utangulizi

Walimu wanahitajika watambue umuhimu wa utaalamu na ujuzi, staidi na mielekeo ya kujifunza. Kuwapa wanafunzi ujuzi ndio kitu kilicho rahisi zaidi, staidi zinachukua muda mrefu wa maandalizi na mazoezi ya kutosha, hata hivyo, jambo lilogumu zaidi ni kubadili tabia na mienenendo ya wanafunzi. Fikiria juu ya mchezo wa soka. Umati wote huwa unajua

mambo muhimu yahusuyo sheria za mchezo huu. Wachezaji wachache ndiyo wajuao staidi za mchezo huu vizuri. Lakini haki, uaminifu na kuheshimiana katika kushindwa ni mienendo muhimu ambayo si rahisi kuipuuza kila mara.

Sehemu hii inatoa utangulizi wa njia mbalimbali za kujenga mwenendo wa uwajibikaji kwa wanafunzi katika matumizi na urejelezaji wa matumizi ya maunzi/rasililimali.

Nyenzo-rejea ya 5: Kuchunguza zaidi hewa