Somo la 2

Kutokana na kazi iliyopita, wanafunzi watakuwa wameanza kuelewa kwamba tunahitaji kufikiri kwa makini kuhusu matumizi ya bidhaa au maunzi yasiyo rejeleka. Tunahitaji kuanza kufikiri jinsi ambavyo tunaweza kujipanga kuwa sehemu ya suluhisho la tatizo na siyo kuendelea kulifanya tatizo kuwa kubwa zaidi. Ni vizuri kuwashirikisha wanafunzi matendo chanya yaletayo manufaa katika mazingira kwa namna fulani.

Katika Uchunguzi kifani 2 , Mwalimu anawahamasisha wanafunzi kwenda kwenye jamii zao na kuangalia athari za watu katika mazingira yao. (Unaweza kujaribu tendo sawa na hili na kama huna karatasi za rangi kuugawa ukuta katika sehemu mbili).

Katika Shughuli 2, tunapendekeza darasa lako libuni, litafiti na kufanyia uchunguzi mradi wa kutengenenza mboji. Unaweza kuanza kwa kueleza zana za maunzi yaozayo na yasiyooza na kuelezea ni nini husababisha vitu kuoza - bakteria. Wanafunzi watakutajia majibu mbalimbali ya mifano ya vitu/ maunzi yaozayo na yasiyo oza. Hili linaweza kuwa tendo la kushirikishana mawazo/majadiliano.

Baadaye unaweza kuendelea kwenye uzalishaji wa mboji kwa ajili ya biashara ambayo itapelekea kwenye njia za ukusanyaji salama wa takataka zinazoweza kuozeshwa kuwa mbolea itakoyouzwa au kutumika katika kulima mboga mboga katika bustani shuleni.

Uchunguzi kifani ya 2: Ushahidi wa Uchafuzi wa Mazingira katika maeneo yaJirani na Mkoani.

Uchunguzi wa vitu hai vinavyozunguka mazingira ya shule kumemfanya Mroki Mroki na wanafunzi wake kuwajali zaidi wanyama na mimea katika mazingira yao. Sasa anajaribu kufanya tendo linalofanana na hilo kuamsha hisia za kuangalia athari za watu katika mazingira ya dunia yetu wa kawaida. Anazungumza na watu kuhusu wazo la ‘unyayo wa mguu’ Wanajadiliana juu ya vitu vyenye madhara na vile visivyo na madhara wanavyoweza kufikiria katika eneo jirani na kwao. Kisha anawapa changamoto kwa kutoa nafasi ya kubandika ‘gazeti’ katika ukuta wote nyuma ya darasa.

Wanafunzi wanakwenda na kuzunguka kwenye maeneo yao kama waandishi wa habari, wakitafuta, kurekodi na kuchora mambo yahusuyo uharibifu wa mazingira. Chochote kile wanachoona kinaharibu au hakisaidii kuhifadhi mazingira wanakiwekea rangi ya udongo. Vile vinavyosaidia mazingira vinapakwa rangi ya kijani na kubandikwa ukutani. Utupaji jicho wa mara moja unaonyesha hali halisi ya eneo lao kwa kuona michoro ya rangi ya udongo = MBAYA na ile ya kijani= NZURI.

Wanafunzi wanapata taarifa nyingi sana kiasi kwamba mabango ya karatasi yanaenea ukuta wa pili. Wanakuja na taarifa za kutoka kwenye magazeti kama magazeti, radio na televisheni kuhusu Tanzania, Afrika na ulimwenguni pia. Michoro ya rangi inaongezeka kila siku na kuanzisha mjadala na ubishani, muhimu zaidi kuhusu tabia ya kujali mazingira.

Shughuli ya 2: Kufanya Tendo zuri kuhusu Utengenezaji wa Mbolea za Taka

Soma Nyenzo rejea 3: Utengenzaji wa Mbolea ya Mboji , huelezea njia moja ya jinsi yakutengeneza.

Waambie wanafunzi wako watafanya mradi wa kutengeneza mbolea kutokana na takataka. Kwanza watahitaji kufanya utafiti juu ya mbolea za taka katika maeneo ya nyumbani kwao kwa vikundi. Ni nini mawazo yao? Je wanaweza kufikiria juu ya mtu yeyote anayeweza kuwasaidia katika eneo lao? Wanaweza kumwalika mtu huyo katika darasa lao au wao kwenda kumtembela mtu huyo?

(Anglia Nyenzo rejea muhimu: Matumizi ya Mazingira

Yanayotuzunguka kama Rasilimali za Kufundishia .)

Kusanya pamoja mawazo yote kutoka kwa wanafunzi juu ya utengenezaji wa Mbolea taka na utafiti wao. Unaweza kuongezea baadhi ya mawazo kutoka Nyenzo rejea 3.

Kisha waulize wanfunzi: Watatumia vigezo gani kupima ubora wa mawazo yaliyotolewa? Wape muda wa kufikiria vigezo watakavyo tumia kwa vikundi.

Shirikiana nao kupata vigezo kisha vitumike kuchuja mawazo yaliyo muhimu. Wanafunzi waandike mawazo hayo kwenye madaftari yao.

Sasa uko tayari kutengeneza mbolea ya mboji. Kila kundi linaweza kujaribu njia tofauti. Usisahau kuwapa wanafunzi muda wa kupanga na kuorodhesha vifaa na kwa kuyapima mawazo yao kutokana na vigezo vya darasa.

Je wanafunzi wako walifurahia kufanya kazi kwa njia hii?