Somo la 3

Wanafunzi wanaweza kugundua njia nyingine za kurejeleza matumizi ya maunzi. Watu waishio jamii masikini wanazo njia nyingi zenye ubunaji na ubunifu kutokana na ulazima. Tafiti za watu wa jamii kama hizi, kama vile Wakhoi-san ( Wakhosa) zimeonyeha jinsi ambavyo hapo zamani hawakupoteza hata kitu kidogo na hivyo walitunza hata unyayo mdogo sana wa binadamu katika ardhi yao kwa heshima kubwa. ( Nyenzo rejea 4: Elimu ya uhusiano wa Viumbe na Mazingira inatoa maelezo ya jinsi ya kutafuta ukubwa wa mguu wako ardhini ). Je sisi tunalingana nao kwa namna gani?

Ni aina gani za urejelezaji unafanyika katika jamii yako? Uchunguzi kifani 3 unaonyesha jinsi mwalimu mmoja na wanafunzi wake wanavyofanya uchunguzi kutafuta vigezo vya kuwepo kwa urejelezaji katika jamii husika.

Katika Shughuli Muhimu , tunapendekeza uwahamasshe wanafunzi wako kufanya zoezi shirikishi la kisayansi na teknolojia. Wafanye kazi ya kuunda na kutengeneza vifaa kutokana na mabaki na kuviuza katika siku maalumu ya ujasiliamali ili kutunisha mfuko kwa ajili ya shule au darasa.

Uchunguzi kifani ya 3: Uchunguzi na changamoto ya urejelezaji

Blossom Namahala aliwashilikisha wanafunzi wake katika kampeni ngumu shuleni. Alihushisha hisabati. Walikusanya uchafu, waliupanga na kuhesabu walichopata. Hili liliwapa data za kuchambua. Waliwasilisha matokeo ya utafiti wao katika mkusanyiko wa shule, wakionyesha grafu na kupendekeza namna ya kutunga sera za uchafuzi wa mazingira.

Alifanya ufuatiliaji wa hili kwa kufanya uchunguzi wa urejelezaji katika eneo lake. Hili pia liliwasilishwa katika mkusanyiko wa shule. Wanafunzi wake walionyesha mipira waliotengeneza kwa kuviriga mifuko ya plastiki, na mifuko ya mikononi na mikoba ambayo wafanyakazi wastaafu wamekroshia terazo za mifuko iliyotumika. Wanafunzi pia walieleza jinsi uzio wa uwanja wa michezo ulivyong’arishwa kwa kuvisha makopo chakavu juu ya nguzo za nyaya.

Mwishowe, Blossom aliwapa wanafunzi wake changamoto: Tunga vigezo vya kujarisha mipira katika mashindano kutengeneza “mipira bora kutokana na mabaki’. (Angalia Nyenzo rejea 5: Vigezo vya kupimia mipira bora kutokana na mabaki .)

Shughuli muhimu: Kutengeneza mazao toka katika mabaki

Hapa tunapendekeza wanafunzi wafanye kazi katika makundi ya kirafiki kufikiri nini watafanya kutengeneza vifaa kutokana na mabaki/uchafu. Vifaa hivyo lazima viwe na umuhimu fulani au viweze kuuzwa katika maonesho baadaye mwaka huo.

Wanaweza kuangalia vifaa vya zamani, kama midoli, ambayo ilikuwa vya muhimu hapo nyuma. Je hivi vinaweza kuboreshwaje? Vipi utengenezaji wa simu za kuchezea watoto? Kama unaweza kuunda mikoba kutokana na mabaki, vipi kuhusu vikombe au mabakuli’?

Ni namna gani unaweza kuwaelezea sayansi inayotumika hapa? Wanapofanya kazi unatakiwa kuwazungukia wanafunzi na kuongea nao katika makundi yao hapo darasani na wamejifunza nini kuhusu maada na vifaa.

Watoe vigezo, au waweze kueleza, namna gani wanaweza kueleza nduni za asili ya mabaki waliyotumia, na kwa nini wamevichagua. Waulize kwa nini wamechagua mabaki hayo. Nduni zao ni nini? Zinatoka wapi? Je vinaweza kurejelezwa au la?

Mwishowe, waambie kila kundi liwasilishe vifaa vyao darasani. Waeleze kwa nini wamechagua baadhi ya mabaki na kama yanaweza kurejelezwa au la?

Nyenzo-rejea ya 1: Rasilimali zinazorejelezwa na zisizorejelezwa