Nyenzo-rejea 3: Kutengeneza mboji

Nyenzo ya Mwalimu kwa kupanga au kubadili nyenzo ili zitumike na wanafunzi.

Njia bora na rahisi ya kutengeneza udongo wa bustani uwe mzuri ni kutengeneza mboji yako. Inahitaji jitihada, muda na kujali kidogo.

Chagua sehemu iliyo karibu na bustani ya shule yenye mwanga wa jua. Toa magugu na uchafu.

Ukiwa na nafasi iliyo wazi, mwanafunzi mmoja anaweza akaweka alama ya mduara kwa kutumia kipenyo cha sm 75. Kama mwanafunzi huyu atasimama katikati ya duara na kugeuka akiwa ameshikilia fimbo ya kutembelea, duara zuri litakuwa limechorwa.

Chukua koleo na chimba shimo katika duara. Chimba kina cha urefu wa koleo. Tumia haratu (rake) kusembua ardhi ndani ya shimo lako.

Weka lundo dogo la udongo karibu na shimo lako kwa kuweka sehemu ya tatu ya udongo wako kutoka katika shimo.

Simika nguzo au tawi nyoofu katikati ya udongo ulio katikati ya shimo lako.

Sasa unaweza kuanza kazi ya kutengeneza mboji. Weka tabaka la matawi na majani ya zamani ulivyokusanya juu ya udongo. Jinsi unavyokuwa navyo vingi ni vizuri.

Kwa kufuatia, weka chini tabaka la vikonyo na mashina ya miti na mabaki ya ya jikoni (maganda ya viazi, mabaki ya majani ya chai, magamba ya mayai). Unaweza kuweka hata mabaki ya karatasi chakavu.

Halafu ongeza tabaka la nyasi zilizokatwakatwa, nyasi kavu au matawi ya kale. Malizia kwa kuweka tabaka dogo la udongo juu yake. Tumia udongo uliotoa katika fungu karibu na tuta lako la mboji.

Endelea kuongeza matabaka:

  • Kwanza vikonyo, mashina, matawi na majani;
  • Halafu mabaki ya jikoni na mabaki ya majani ya kijani,
  • Halafu majani makavu, majani ya kale na mboji (kama utapata);
  • Malizia mwisho wa kila tabaka na udongo.

Nyunyiza maji kidogo – lakini hakikisha tuta la mboji halilowi sana. Ukubwa utapungua jinsi mboji itakavyooza. Halafu unaweza kuongeza

matabaka mengine kwa vipindi rasmi. Wakati wote weka tabaka la

udongo juu – hii hupunguza wadudu warukao.

© Mboji ya Bustanini 2007

Nyenzo-rejea ya 2: Mazao ya mafuta machafu

Nyenzo-rejea ya 4: Ekolojia ya Unyayo wa miguu