Nyenzo-rejea ya 5: Andalio la somo: Kutafuta mpira bora uliotengenezwa na mabaki
Nyenzo ya Mwalimu kwa kupanga au kubadili nyenzo ili zitumike na wanafunzi.
Ni vema ukiwasaidia wanafunzi wako kufikiri namna ya kuamua mpira ulio bora kabla ya kutengeneza mpira wa mabaki salama na usafi.
Kwanza, anza na chemshabongo ambayo wewe na wanafunzi mtaweka vigezo vya mpira ulio bora. Tegemea majibu kama:
- Mpira bora ni:
- mviringo mzuri na ukubwa bora;
- huviringika vema;
- unadunda vizuri;
- imara;
- mlaini kudaka.
Wanafunzi waweza kuwa na mawazo zaidi – orodhesha ubaoni.
Pili, wewe na wanafunzi wako mnatakiwa kujadiliana jinsi ya kuweka vigezo vya uzuri wa mpira.
Mviringo mzuri na ukubwa sawa: Je mpira unatosha vizuri katika tundu mviringo la waya au kadibodi lenye mzingo/ kipenyo sawa ukiuweka namna yoyote ile? Je waweza kuushika vizuri?
Huviringika vizuri: Pima uwezo wa kuviringika – muamue umbali katika mstari.
Hudunda vema: Mnatakiwa kuuangusha mpira kutoka urefu sawa na mpime mdundo kwa kila mpira na mlinganishe.
Imara: Hii itajaribiwa kwa matumizi ya kweli. Kwa kiasi gani mpira unahitaji kurekebishwa au kubadilishwa?
‘Unadaka kirahisi’: Je unaumiza ukidaka?
Mwishowe, unahitaji kuweka alama na kuangalia kama alama zinafaa
(mfano umewekwa chini).
Utatakiwa kuweka hizi alama katika karatasi ubaoni na wanafunzi. Unaweza kugawa darasa katika makundi – kila kundi na amana ya alama.
ALAMA KWENYE MPIRA | 5 | 4 | 3 | 2 | 1 |
---|---|---|---|---|---|
Sura na ukubwa | Hufaa kwa mdundo | Hufaa kidogo kwa mdundo,pungufu ya | Hufaa kidogo kwa mdundo, pungufu ya | Haufai | Haufai kabisa |
Huviringik a vema | Hufaa katika eneo tambarare | Pungufu kwa sm | Pungufu kwa 5–10 nje ya mstari | Pungufu kwa | Nje ya mstari kabisa |
Hudunda katika m1.5 | Kama m 1 | Zaidi ya sm 50 | Kati ya sm 25–50 | Kama sm10–25 tu | Haudundi kabisa |
Mgumu- hudumu muda gani | Hudumu dakika 10 | Hudumu dakika 5–10 | Hudumu dakika 2–5 | Hudumu dakika 2 | Haudumu hata kwa dakika 1 |
Rahisi kushika | Hushikika kirahisi bika kuumiza | Huumiza kidogo | Huumiza kidogo hapo hapo | Huumiza kidogo kwa mikwaruz o | Huharibu mikono |
Lipe kila kundi muda wa kutafuta vifaa na kutengeneza mipira yao.
Sasa watake kila kundi kupima mipira yao kwa kutumia vigezo mlivyovitengeneza. Wamepata alama gain kwa kila kigezo? Wamepata alama ngapi kwa jumla?
Unaweza kuta wewe na wanafunzi wako mnatakiwa kubadilisha vigezo kila watakapotengeneza mipira yao. Hii itaonyesha kuwa wanaonyesha jinsi wanavyoweza kufikiri kimantiki. Wanaweza kufikiri hata jinsi ya kuongeza vigezo, mfano, mwonekano. Hili pia lahitaji kupongezwa.
Nyenzo-rejea ya 4: Ekolojia ya Unyayo wa miguu