Nyenzo-rejea ya 4: Mhutasari wa nguvu kwa mwalimu
Maarifa ya msingi/welewa wa somo wa mwalimu
- Nguvu ni mvutano na msukumo
- Nguvu ina tabia mbili: ukubwa na uelekeo
- Nguvu zikiwa vinafanya kazi, zinaweza kubadili umbo la vitu. Kuna badiliko kubwa kutokana na nguvu kubwa.
- Tunaweza kutumia mabadilko kutoa kipimo cha nguvu iliyotumika.
- Nguvu zinaweza kupimwa kwa mizani mneso au mita ya nguvu (Newton-mita)
- Uzito wa kitu ni nguvu ya dunia ya mvutano na dunia, hivyo uzito ni nguvu.
- Masi ya kitu ni kipimo cha kiasi cha mada ilichonacho. Masi hubaki ileile, haibadiliki
- Vitu vyote huwa na nguvu dhidi ya vitu vingine, kiasi cha nguvu hutegemea masi yake
- Msukumo wa dunia ni nguvu tushikiria
- Nguvu ya mvutano wa dunia ni ndogo kwenye mwezi kuliko katika dunia kwa sababu kuna maada kidogo kwenye mwezi (masi chache) kuliko ilivyo kwenye dunia.
- Katika dunia, kila kilogram moja huvutwa na mvutano wa nguvu inayokadiliwa kuwa nyuton 10 kuelekea katikati mwa dunia.
- Kuna utofauti kati ya masi na uzito. Masi ni sifa ya ndani ya kitu fulani-haijarishi upo wapi, daima unakuwa na masi ileile. Uzito wako ni nguvu ya uvutano na dunia inayofanya kazi kwako. Uzito wako hugandamiza kwenda chini, kuelekea katikati mwa dunia
- Masi na uzito vina uzio tofauti. Masi hupimwa kwa gramu na kilogramu wakati uzito hupimwa katika nyutonsi (Newtons).
- Msuguano ni nguvu inayofifisha mwendo.
- Nguvu huhitajika kufanya kitu kianze kujongea, kuongeza kasi, kupunguza mwendo au kubadili uelekeo
- Kadri nguvu inavyokuwa kubwa ndivyo kima cha badiliko la mwelekeo huwa kikubwa
- Kusipokuwa na nguvu yoyote inayokisukuma kitu, kitabakia kimetulia au kuendelea katika kasi ileile katika msitari mnyofu.
Chanzo Asilia: kukuza ujuzi katika somo – Jane Devereux
Nyenzo-rejea ya 3: Mnyambuliko wa maneno ya nguvu.