Nyenzo-rejea ya 2: Mawimbi ya sauti- nyaraka za mwalimu
Taarifa za msingi/ welewa wa somo wa mwalimu
Sauti ni nini?
Sauti hutokea pale vitu vinapotetema. Kitu kinaweza kuwa waya wa gitaa, sehemu bapa kama ngozi za ngoma, kiwambo katika spika au hata
kamba nyembamba za sauti.
Sauti husafirisha nishati kutoka kwenye kitu kinachotetema, na huhitaji kitu fulani cha kupitia. Sauti haiwezi kusafiri kwenye ombwe tupu-katika nafasi, hakuna mtu atakaye kusikia upigapo mayowe!
Mwendo wa sauti
Sauti husafiri katika mwendo tofauti kupitia dutu/kitu tofauti tofauti. Kwa ujumla, kadili dutu inavyokuwa nene/nzito ndivyo sauti husafiri kwa haraka. Sauti husafiri kwa mwendo wa mita 5100 kwa sekunde kupitia chuma, m1480 kwa sekunde kwenye maji na mita330 kwa sekunde hewani. Hii ni pungufu ya mwendo wa mwanga.
Mwanga husafiri takribani mara milioni zaidi ya sauti kupitia hewani. Ndio maana unasikia muungurumo wa radi baada ya kuona miale ya radi
katika mvua za radi, na ndio sababu sauti ya mlio wa nyundo katika umbali fulani hailingani na mgongo wa nyundo yenyewe.
Mwangwi
Sauti inaweza kuakisi kutoka kwenye sura ya kitu fulani. Huu unaitwa mwangwi. Sura ngumu huakisi vizuri zaidi kuliko sura laini.
Ukubwa wa Sauti
Ukubwa wa sauti hutegemea ukubwa wa mitetemo. Mitetemo mikubwa husafirisha nishati zaidi kuliko mitetemo midogo, hivyo ina sauti kubwa.
Uzito wa sauti
Sauti inaweza kupangwa kutoka sauti nzito hadi nyembamba. Uzito wa sauti hutegemea namna mwendo wa chanzo cha sauti hizo. Kama mitetemo kwa sekunde ni mingi, kasi ya mawimbi ni kubwa na sauti ina uzito wa juu. Kama mitetemo kwa sekunde ni michache kasi ya mawimbi ni ndogo na sauti itakuwa ya chini
Sehemu ya tathmini ya sauti
Kusikia
Tunasikia kwa sababu mawimbi ya sauti huingia masikioni na kusababisha ngoma ya sikio kutetema. Mifupa mitatu ndani ya sikio hupeleka
mitetemo kwenye kongoli. Kongoli lina vinywele vidogo vidogo, vinapotetema hupeleka ujumbe kwenye.
Kuharibika kwa usikivu
Usikivu wetu huharibiwa kiurahisi na kadri tunavyozeeka inakuwa vigumu kusikia sauti za chini au za juu. Mifupa hiyo mitatu inaweza kuungana pamoja kadri umri unavyoenda, kwani siyo nzuri sasa kupeleka mitetemo kutoka kwenye ngoma ya sikio kwenda kwenye kongoli.
Sauti kubwa hatimaye zinaweza kuharibu usikivu wetu. Kama ngoma ya sikio imeharibika, inaweza kujitengeneza yenyewe tena, lakini kama kongoli limeharibika, unakuwa ni ulemavu maisha. Watu wenye matatizo ya kusikia wanaweza kupata ugumu wa kufuatilia mazungumzo na wanaweza kuhitaji misaada ya kusikia.
Chanzo Asilia: BBC World, Website
Nyenzo-rejea ya 1: Hadithi za sauti