Nyenzo-rejea 5: Zana asili za muziki

Taarifa za msingi/ welewa wa somo wa mwalimu

Tanzania inaidadi kubwa ya zana za asili, nyingi ya hizo ni za makabila fulani. Wazaramo kwa mfano, hucheza dansi yenye tuni asili kama

Mitammba Yalagala Kumchuzi’.

Gitaa la asili ilikuwa ni fidla kubwa yenye mwangi uliotokana na kifuu cha nazi na hiki ni kitu cha kawaida pwani. Marimba ni zana ya muziki inayojulikana na makabila mengi, hasahasa yanayozunguka Dodoma. Kiboksi kidogo cha mbao ndicho kitoacho sauti za nyuzi za urefu tofauti tofauti, ambazo huguswa kwa dolegumba kutoa muziki.

Ngoma ni zana maarufu ya muziki wa Afrika. Kuna aina mbalimbali za ngoma, zenye umbo na saizi tofauti. Pia ngoma zilitumika kwenye matukio muhimu ya asili kama matangazo ya kuwasili au kuondoka kwa kiongozi wa kabila fulani au kuwapa motisha kwa jamii za wakulima kupitia dansi iitwayo Gobogobo. Baadhi ya ngoma zilitumika kuwakusanya watu ili kuonana na kiongozi wao au kujulisha vita/mapigano.

Mtaalamu wa zana asili Hukwe Zawose, wa kabila la Wagogo, alikuwa maarufu Tanzania kwa muziki wa asili katika karne ya 20. Alijikita kwenye

‘ilimba’, zana moja kubwa inayofanana na mbira.

Imenukuliwa kutoka: Tanzanian Embassy and Tanzanian Music Wikipedia, Website

Kama unaweza kupata mtandao, unaweza kumsikiliza Dumisani Mariare akiimba na kucheza mbira, fungua http://trumpet.sdsu.edu/ M345/ mp3/ Chaminuka.mp3 [Tip: hold Ctrl and click a link to open it in a new tab. (Hide tip)]

Nyenzo-rejea 4: Dhana ya kutathmini zana

Sehemu ya 3: Kuchunguza umeme