Nyenzo-rejea 4: Kadi za kazi
Nyenzo ya Mwalimu kwa kupanga au kubadili nyenzo ili zitumike na wanafunzi.
KADI YA KAZI 1: JOTO
Unakuwa na:
Betri ya tochi/balbu ya tochi
Waya mtupu mwembamba wa urefu wa sm 10 wa fyuzi
Waya mtupu wa kawaida wa shaba wa urefu wa sm10
Unachofanya:
- Shika waya wa sm 10 ncha zake moja ikiwa juu na nyingine chini ya betri.
- Gusisha mkunjo wa waya nyuma ya kiganja cha mkono wa mtu. Anahisi chochote?
- Rudia kwa kutumia waya mwembamba/au waya wa fyuzi. Anahisi kitu chochote sasa?
- Hapa unahisi aina gani ya nishati?
- Jadili juu ya ulichohisi. Jaribu kufikiria maelezo yako mwenyewe. Jaribu kwa kutumia nyaya tofauti kuwasha balbu. Linganisha ung’avu wa mwanga. Unafikiri nini?
KADI YA KAZI 2: USUMAKU
- Unakuwa na:
- Betri ya tochi
- Waya wa shaba wenye urefu wa sm 30 uliofunikwa
- Msumari mkubwa laini wa chuma
- Baadhi ya vitu vya metali-pini,nk.
- Unga wa chuma
- dira ndogo
Unachofanya:
- Kwanza angalia kama msumari mkubwa laini wa chuma una madhara yoyote kwenye pini, dira.
- Kunja waya kuzunguka msumari mara nyingi.
- Shikisha ncha mbili tupu za waya kwenye ncha mbili za betri
- Wakati waya umejishikiza, angalia kama kuna madhara kwenye pini, n.k
- Ni aina gani ya nishati unapata?
- Unaweza kufanya ncha moja ya msumari isukume upande mmoja wa dira?
- Nini maelezo ya kikundi chako juu ya ulichokiona hapa?
KADI YA KAZI 3: MWENDO
Unakuwa na:
- Betri ya tochi
- Waya wa shaba uliofunikwa wenye urefu wa sm 25
- Pini ambayo ina usumaku (imefanywa kuwa sumaku kwa kuwekwa pamoja na sumaku kwa muda)
- Kipande cha kadi nyembamba inayojikunja ya sm 15
- Mota ndogo ya umeme inayotokana na mwanasesere aliyeharibika au redio
- Pini ya kuchorea
Unachofanya:
- Zungusha waya kwenye penseli kutengeneza mzingo.
- Funga kipande cha kadi kwenye pembe ya meza/dawati ionekane kama ubao ya kuogelea kwenye bwawa la kuogelea.
- Sukuma pini yenye usumaku ili ining’inie wima kwenye ncha moja ya kipande cha kadi.
- Shika mzingo sawasawa huku pini ya usumaku ikining’inia katikati mwa mzingo.
- Shika betri ya tochi huku ncha moja ya waya kutoka kwenye mzingo ikigusa sehemu ya chini ya betri.
- Mtu mwingine hivyo hivyo anagusisha ncha ya pili ya waya upande wa juu wa betri.
- Jadili kitu ulichoona kinatokea. Ni aina gain ya nishati unaipata? Nini maelezo ya kikundikuhusu mlichokiona?
- Sasa, igeuze betri juu-chini na urudie zoezi hilo. Lakini kwanza TABIRI kitu utakachokiona.
- Mwisho – tumia betri ya tochi kutengeneza mota ndogo ya umeme. Unazungusha kuelekea upande gani? Unaweza kubadilisha mwelekeo?
- Unadhani mota ya umeme inahusiana na mizingo ya nyaya uliofunikwa na sumaku?
KADI YA KAZI 4: SAUTI
Unakuwa na: Betri ya tochi
Spika ndogo kutoka kwenye kifaa cha umeme kikuukuu kilichoharibika
Mchanga mkubwa/vipande vya nyaya zinazojikunja
Unachofanya:
- Fanya jaribio kuona kama unaweza kupata sauti kutoka kwenye spika kwa kugusisha ncha za betri na spika (kwanini mara zote huwa mbili?).
- Inakubidi uweze kupata sauti kali.
- Unatakiwa ufanye nini ili sauti irudie?
- Sambaza mchanga mkavu juu ya koni ya spika iliyo wazi. Unagundua nini unaporudia kutoa sauti kali?
- Ziangalie spika kwa makini. Unaweza kuona mipangilio yoyote ya sumaku na mizingo au mizunguko ya nyaya?
- Jadili mtazamo wako mwenyewe namna spika zinavyofanya kazi.
- Unaweza kuunganisha mtazamo wako na kadi ya kazi 3: Mwendo?
KADI YA KAZI 5: MWANGA
- Unakuwa na:
- Betri tatu za tochi
- Balbu nne za tochi
- Nyaya za kukunjika zenye urefu mbali mbali
- Tayari umeshaona jinsi tunavyowasha balbu na tayari umeshachunguza mfumo wa balbu ya mwanga.
Unachofanya:
- Chunguza mipangilio mbalimbaIi ili upate idadi mbalimbali ya betri za tochi kuwasha idadi mbalimbali ya balbu.
- Andika mipangilio mbalimbali inayofanikiwa. Chora picha kuonyesha mipangilio hiyo.
- Ni balbu zipi zilitoa mwanga mkali sana?
- Unaweza kufikiria kuelezea ulichokiona?
Nyenzo-rejea 3: Dhana ya kutathmini zana