Somo la 2
Kuujadili ufundi wa mahali hapo au silaha za asili au mavazi inahamasisha sana kwa wanafunzi walio wengi kwa kuwa wanaweza kuona uhalisia wa vitu hivi katika maisha yao.Wanafunzi wanapovutiwa, inakuwa pia ni rahisi kwako kusimamia tabia zao. Kwenye Uchunguzi kifani 2, kuvutiwa huku kunasababishwa na mgeni. Unamfahamu mtu yeyote ambaye ana muda wa kutembelea darasa lako? Umewauliza wanafunzi kama kuna mtu yeyote wanamfahamu?
Vilevile kama unatumia zaidi njia shirikishi kama vile, kuwagawa wanafunzi wawili wawili au katika makundi, wanafunzi wanaweza kuelewa zaidi kwa kufanya kazi pamoja. Katika Shughuli 2, wanafunzi wanafanya kazi wawili wawili kutafuta majibu ya maswali yao wenyewe. Hii nayo pia inawapa motisha sana wanafunzi.
Uchunguzi kifani ya 2: Kuangalia historia ya zana asilia za kilimo
Bwana Msane aliwataka wanafunzi wake kutafuta habari zaidi kuhusu zana za asili zinazotumika kwa kilimo. Aliamua kuwapa nafasi ya kuangalia picha na ughushi, na kuandika juu ya walichokiona. Lakini kwanza,alilishangaza darasa lake. Alikuwa amemuomba mwanajamii mmoja ambaye alikuwa na mkusanyiko wa zana za asili kuzileta baadhi yake darasani.
Wanafunzi waliufurahia huo ugeni na waliweza kukusanya habari nyingi kuhusu zana za asili na kuongezea katika utafiti wao. Koleo la zamani ambalo lilikuwa la babu yake na mgeni liliwasisimua sana wanafunzi hasa kwa sababu ya umri wake mkubwa.
Baada ya ugeni, Bwana Msane aliligawa darasa lake katika makundi madogo na kuwapa kila kundi picha –baadhi ya makundi yalichangia picha moja kwa kuwa hakuwa na picha nyingine za kuwapa.Aliwaeleza kuwa walitakiwa kuzijadili hizo picha na baadae kuandika habari fupi kuhusu kila zana ya kwenye picha ilivyokuwa ikitumika.
Alieleza kuwa wangeweza kutumia karatasi ya maswali na kufikiria juu ya kitu gani cha kuandikia (angalia Nyenzo rejea ya muhimu 1: maswali ya utafiti kuhusu zana za asili ). Wanafunzi walitumia muhtasari wao kutoka kwa mgeni na pia kutoka kwenye baadhi ya vitabu ambavyo Bwana Msane alikuwa anavyo. Walifanya kazi pamoja kwenye makundi yao na kuandika. Mwishoni, kila kundi lilitoa lilichoandika kwa darasa zima.
Shughuli ya 2: Kutafiti ufundi wa mahali hapo
Waambie wanafunzi, wawili wawili, wachague ni zana zipi wanataka kuzitafiti zaidi.
Kila kundi la wanafunzi wawili wawili linaweza kuchagua kati ya kutafuta maelezo kwenye vitabu au kumhoji mtu katika jamii yao, ikiwa ni hatua ya kuanzia.
Halafu, waambie wafikirie aina ya maswali wanayouliza ili yawaongoze wapate maelezo sahihi, kama vile: “Nini matumizi ya asili ya hili bakuli?” Jadili baadhi ya majibu na muamue kwa pamoja kama yanatoa mwelekeo kuhusiana na lengo la utafiti. Kila kundi la wanafunzi wawili lichague maswali yake.
Kila kundi lifanye utafiti kwa kutumia maswalli yake, na njia yao ya utafiti waliyochagua. Kwa wale ambao watatumia vitabu kama vyanzo vya habari, utahitaji kutoa vitabu au makala kutoka vitabuni au magazetini, na wengine uwape muda wa kufanya mahojiano.
Kama wanapata tatizo la kupata habari kwa kutumia njia moja, wanaweza kutumia njia nyingine vilevile. Wape muda wa kutosha kwa ajili ya utafiti na waongoze wanapopata ugumu.
Waambie kila kundi watengeneze bango ili kuonyesha majibu yao
Tathmini kazi ya wanafunzi wako kwa kutumia Nyenzo rejea ya muhimu 2: Karatasi ya kutathimini mawasilisho ya utafiti .
Somo la 1