Somo la 1
Kuwasaidia wanafunzi wako watambue thamani ya ngoma za kimila za Kiafrika ni sehemu muhimu ya kufundisha sanaa. Kujifunza kuhusu sanaa mara nyingi kumejikita katika masimulizi ya zamani.
Pia, sanaa inawawezesha watu kuelezea maana katika maisha yao ya kila siku na kuwasaidia kujenga hisia za kujitambua na kujithamini.
Uchunguzi Kifani 1 na shughuli 1 itakusaidia kuzingatia pamoja na wanafunzi wako namna mila zinavyobadilika na kutoweka, na mdahalo iwapo hili ni jambo zuri au baya.
Uchunguzi kifani ya 1: Kuchunguza Wavenda na domba
Bi. Sylvia Msane anafundisha katika shule ya msingi Sebokeng, mji ulioko kusini mwa jiji la Johannesburg Afrika Kusini.
Sylvia ameolewa na mwanaume mwenye asili ya Kizulu na wanaongea kiingereza na Kizulu nyumbani. Hata hivyo, mababa wamama yake wanatoka venda. Sylivia anahusisha kwamba wanafunzi wake kama walivyo vijana katika Afrika kusini, wanajua kidogo kuhusu vyanzo vya kimila. Sylvia anafikiria msemo uliorithishwa kwake ‘Umuntu ngu muntu nga bantu’ ‘Mtu ni mtu kwa sababu ya watu wengine’
Ameamua kuwaambia wanafunzi wake hadithi ambazo bibi yake alimhadithia alipokuwa mtoto kuhusu watu wa Venda (angalia nyenzo rejea muhimu 1: Hadithi za ngoma za Wavenda). Baada ya kuwaeleza namna watu wa venda walivyokuja kuishi kaskazini mwa Afrika ya Kusini, anawaonyesha nguo za kimila za kivenda na picha ya mabinti wakicheza domba. Mwanafunzi mmoja anauliza wanachofanya hao wanawake. Sylvia anafafanua kuwa hawa wanawake ni kama wamemaliza kufundwa/jando na wanacheza kama nyoka.Anawaeleza hadithi nyingine kuelezea umuhimu wa nyoka huyu na wanagundua namna ya ngoma ya domba inavyosherekea uwezo wa kuzaa wa mabinti (angalia nyenzo rejea muhimu 1). Mwanafunzi mwingine alimuuliza kama alifundwa katika njia hii na anaelezea kuwa hakufanyiwa hivyo. Maisha ya watu na vipaumbele vimebadilika na mila nyingi tokea zamani zimekufa. Wanajadili iwapo ni vizuri au vibaya kwa hili lililotokea.
Nyenzo rejea ya muhimu 2 : Mila za kienyeji inakueleza kuhusu mitindo ya ngoma katika Tanzania.
Shughuli ya 1: Kuchunguza ngoma za asili za Kiafrika hapo zamani.
Chunguza kutoka darasani mwako, wanafunzi wenzio au wanajamii kama kuna wachonga ngoma za asili katika eneo.
Muulize mwalimu mkuu kama unaweza kumwalika mtu. Wasiliana na mtu na mwalike aje azungumze na darasa lako juu ya ngoma za asili na utoe mfano wa ngoma moja au mbili.Waambiwe waje na nguo wanazovaa.
Andaa darasa lako kwa ajili ya ugeni (angalia nyenzo ya muhimu: kwa kutumia jumuiya/mazingira kama nyenzo rejea ). Fikiria kuhusus maswali ambayo wanafunzi wanaweza kutaka kuuliza.
Andaa darasa lenye nafasi kwa mgeni kukaa na kucheza ili wanafunzi wote waone.
Mkaribishe na kumtambulisha mgeni.Mgeni aongee na kucheza kwa takribani nusu saa.
Wahimize wanafunzi wako kumuuliza mgeni maswali.
Baada yaugeni, jadili na wanafunzi wako walivyojifunza kuhusu ngoma. Nani wameipenda? Nani wanapenda kufanya zaidi/Kuendelea? Fikiria cha kufanya baadaye.Labda mgeni atarudi kuwafundisha baadhi ya ngoma?
Sehemu ya 3: Kutumia ngoma kujifunza