Somo la 2
Kucheza ngoma darasani kunafaa kwa kazi za mtaala, kwani unagundua mawazo ndani ya ngoma, umuhimu wa mavazi (maalumu) na kujifunza namna ya kucheza ngoma.
Ngoma ni shughuli halisi na inaweza kufanywa kama sehemu ya elimu ya viungo au inaweza kutumika kugundua mawazo katika maeneo ya masomo mengine kama vile fasihi na sayansi.
Katika uchunguzi kifani 2 na shughuli 2 za ngoma inatumika kuwasaidia wanafunzi kuonyesha kile wanachojua juu ya mada au kuhadithia hadithi.
Uchunguzi kifani ya 2: Kufanya kazi kwenye makundi ili kutengeneza mpangilio wa ngoma.
Bibi Msane amekuwa akifanya kazi na darasa lake namna ubongo anavyotuma ujumbe mwilini. Anaamua kutumia mada hii katika masomo yake ya PE ambapo anafanya mfululizo wa masomo juu ya ngoma.
Bibi Msane anawaambia wanafunzi wake kuwa atawagawanya katika makundi ya watu kati ya sita na kumi. Kundi linatakiwa kufikiri njia za kuonyesha namna ujumbe unavyokwenda kutoka kwenye ubongo mpaka kwenye sehemu ya mwili kuiambia ijongee na ujumbe mwingine kurudi
kwenye ubongo kujenga au kusimamisha mjongeo. Anawapa muda wa kufikiri juu ya hili na anawazungukia kuwasaidia wanapozungumza.
Baada ya dakika 15, anapendekeza wanavyofikiri namna ya kucheza ngoma na kuanza kufanya kwa vitendo.Anawatahadharisha/anawakumbusha kuwa waeneze ujumbe/mawazo yao kwa myumbo bila maneno.
Baada ya kufanya kwa vitendo kila kundi linaonyesha namna lilivyofanya baada ya kila tukio/Sehemu ya darasa iliyobaki wanatakiwa kubuni kinachotokea na wanaweza kuuliza maswali.
Anaamua kuwapa muda wa kujenga mawazo yao na kuyaonyesha kwa darasa juma linalofuata, kundi moja mwishoni mwa kila siku.
Bibi Msane anagundua kuwa kila mmoja amefurahia na anafikiri kwamba wanafunzi wake pia wanafahamu umuhimu wa ngoma kama nyenzo ya kujieleza na kama njia ya kuwasiliana.
Shughuli ya 2: Kutumia ngoma kutoka zamani mpaka sasa kuwasiliana.
Kumuulizia kila mwanafunzi kutafiti ngoma ambayo mzazi ndugu au mtu wa makamo alikuwa akicheza au bado anafanya. Siyo lazima iwe ngoma ya asili.
Watambue
Ngoma inatoka wapi?
Kwa nini ngoma ilichezwa na ilikuwa na lengo gani? Ilichezwa wapi?
Namna ilivyochezwa?
Wape nafasi ya kufanya hivyo na kuadika namna ya kucheza ngoma (angalia pia nyenzo muhimu rejea: kutafiti darasani )
Kinachofuata, kwa kutumia moja ya ngoma za asili kama msingi, waulize wanafunzi wako kuorodhesha inachokusudia (ngoma) kuonyesha)
Sasa waambie wanafunzi wako kuandaa ngoma zao wenyewe kwa kutumia mbinu yoyote wanayopenda, kueleza mawazo yanayofanana. Haya yanaweza kuwa yanahusu.
Kufikia utu uzima; Kuzaliwa kwa mtoto; Mavuno mazuri
Wape nafasi ya kutenda na kushiriki katika ngoma zao
Wakumbushe wanafunzi wako kuwa wanatakiwa kuonyesha hisia zao; kama vile furaha, dukuduku, mshtuko, huzuni pamoja na miili yao na nyuso wanapocheza.
Jadili hisia hizi na wape muda wa kufanya mazoezi tena. Shiriki nao utendaji tena na jadili namna walivyoboresha.
Somo la 1