Somo la 3

Ngoma inaweza kuwa na mvuto kwa mtu binafsi lakini pia imejikita kwenye uchezaji wa kikundi na kuwaruhusu wanafunzi wako wakue katika

kujiamini na kujithamini.. Hii ni muhimu kwani inaweza kuinua mtazamo wao juu ya kujifunza na mafanikio yao.

Kama mwalimu, ni muhimu katika nafasi ya vitendo kutambua watu katika kundi na mafanikio yao, pamoja na mafanikio ya pamoja ya kundi.

Uchunguzi kifani 3 na shughuli muhimu 3 inapendekeza njia za kutoa mrejesho kwa wanafunzi wako utakaowasaidia kujiandaa kucheza mbele ya hadhira. Utagundua pia namna rika linavyoweza kupima na kupeana mwisho nyuma ili kujenga uelewa wao na kuboresha kazi zao.

Uchunguzi kifani ya 3: Kuandaa na kutoa burudani ya ngoma kwa mafanikio.

Bibi Msane anasikia kutoka kwa mmoja wa washiriki kwamba shule itakuwa na siku ya wazi mwishoni mwa muhula. Wazazi na watu kutoka kwenye jumuiya wataalikwa kuhudhuria. Bibi Msane amevutiwa na shauku ya wanafunzi wake kutokana na kazi ya kucheza ngoma waliyokuwa wakifanya na anaamua kuwasaidia kutengeneza/kuendeleza ngoma walizotengeneza darasani ili zichezwe kwenye ‘Siku ya Wazazi’ (Open Day).

Anawahimiza kufanya mazoezi wakati wa chakula cha mchana na kutenga muda wakati wa masomo ya elimu ya viungo. Juma moja kabla ya ‘siku ya wazazi’, wanacheza wenyewe kwa wenyewe na kutoa mrejesho juu ya ubora wa ngoma na njia za kuboresha. Anatumia mfululizo wa maswali kuwasaidia kufikiri juu ya kuboresha uchezaji wao (angalia nyenzo rejea 3: Kuboresha ngoma yetu ). Wanafanya mazoezi na kukamilisha ngoma yao. ‘Siku ya wazazi’, kila mtu alishangaa namna wanafunzi wa Bibi Msane walivyofikisha mawazo kuhusu namna akili inavyofanya kazi kwa kutumia ngoma. Hatimaye, bibi Msane anawaambia kutafakari uzoefu walioupata; hii inampa mrejesho wa kufaa juu ya mchakato wa kujifunza, pia kuwasaidia wanafunzi wake kufikiri juu ya kile walichopata (angalia nyenzo rejea 4: Tafakari juu ya ngoma).

Shughuli muhimu: Kujiandaa kucheza

Kabla ya somo la kwanza, soma nyenzo rejea 3 na 4

Waeleze wanafunzi wako kuwa watacheza ngoma jioni inayofuata kwa wazazi na kwamba mwalimu mkuu anaalika wanajamii pia waje.

Kabla hujaanza hakikisha kuwa wanafunzi wako wanajua mahitaji ya kuwa waangalifu. Wape maelezo ya kina namna utakavyokuwa unawasimamisha wanapocheza na watahadharishe kuwa wanapaswa kujua walipo wanadarasa wenzao.

Panga darasa lako latika makundi.Kiambie kila kikundi kuandaa ngoma kulingana na mada walizokuwa wanasoma. (Unaweza kuamua au waruhusu wanafunzi wapigie kura kutoka kwenye orodha.

Yape makundi muda wa kufanya mazoezi.

Ruhusu kila kikundi kucheza mbele ya darasa. Wahamasishe wanafunzi wako kupeana yanayofaa yatakaowasaidia kuboresha michezo yao.

Wasaidie wanavikundi wanapofikiria namna ya kuboresha na kuziremba ngoma zao ili ziwe tayari kuchezwa mbele ya hadhira

Jadili mavazi na vivaa vya ngoma na uviandae

Andaa ratiba

Cheza

Jadili pamoja namna ilivyoenda. Wamejifunza nini kuhusu ngoma? Wamejifunza nini juu ya mada?

Nyenzo-rejea ya 1: Hadithi za ngoma ya Venda