Somo la 1
Mazingira ni nyenzo ya thamani katika kugundua sauti na namna vifaa tofauti vinavyoweza kutoa sauti.
Madhumuni ya sehemu hii ni kupanua uelewa wa wanafunzi wako na uzoefu wa aina mbalimbali za sauti, na kuona namna wao wenyewe na mazingira yao ya karibu yalivyo nyenzo za muziki. Uchunguzi kifani 1 na shughuli 1 vinaonyesha namna sauti katika maisha yetu ya kila siku zilivyo mwanzo mzuri wa mada hii.
Shughuli hizi zingeweza kupanuliwa kwa kuwaambia wanafunzi watengeneze zana zao wenyewe kutokana na vifaa vya kawaida* (makopo, chupa n.k) au unaweza ukabahatika kuwapata wanafunzi wanoweza kupiga zana au kuimba. Wapangie namna watakavyoonyesha ujuzi wao darasani.
Angalia Nyenzo rejea 1: Kugundua sauti ili kupata taarifa za msingi na moduli ya SAYANSI 3, Sehemu ya 2 kwa taarifa zaidi juu ya sauti na vifaa vya muziki.
Uchunguzi kifani ya 1: Kutengeneza ramani akilini kuunganisha vifaa na sauti
Katika darasa lake la msingi la Soweto, Afrika ya Kusini, Bi Simelane anagundua wavulana wawili wakigonga dawati. Anasikiliza kwa makini jinsi wanavyotengeneza mapigo kwa kutumia dawati kama ngoma. Halafu wanagonga makasha yao ya penseli. Bi Simelane anafuatilia kwa makini muziki wao, na anawaambia wanadarasa wafumbe macho yao na
kusikiliza. ‘Wanatengeneza muziki? Kwa jinsi gani?’ ‘Unaweza kusikia
sauti gani tofauti?’ Wanafunzi wanavutiwa kutumia madawati yao, kalamu zao na makasha ya penseli kutengeneza sauti. Anawaacha wagundue sauti tofauti wanazoweza kutengeneza kwenye madawati yao kwa kutumia vifaa vinavyowazunguka. Wanasikiliziana sauti na kutoa maoni ya jinsi zinavyotengenezwa.
Bi Simelane anawaambia wanafunzi wapendekeze zana zinazotengeneza sauti akilini mwao na kuzirekodi ubaoni. Anawahimiza kufikiria juu ya uhusiano kati ya vifaa na sauti. ‘Ni aina gani ya sauti tunaisikia tunapogonganisha chupa na kijiko? Au kupuliza mdomo wa chupa ulio wazi?’ ‘Ni sauti gani zinatengenezwa na ngoma za ukubwa tofauti?’
‘Tunailezeaje sauti?’ anaongezea mawazo yao kwenye ramani ya akilini mwao.
Anaridhishwa na majibu yao na anaona huu kama ni mwanzo wa wanafunzi kutengeneza zana zao kwa kutumia vifaa vilivyo kwenye maznagira ya kawaida. (Angalia Nyenzo rejea 2: Kutengeneza zana ).Mwishoni mwa somo, anawaambia waende nyumbani na kukusanya vifaa vingi tofauti kadri watakavyoweza na kuvileta shuleni kuongezea kwa vile vilivyokwisha kusanywa. Juma lijayo watatengeneza na kuonyesha zana hizi.
Shughuli ya 1: Kusikiliza sauti
Kabla ya somo, soma Nyenzo rejea 3: Kusikiliza sauti katika maisha ya kila siku.
Waambie wanafunzi wako wakae kimya na kusikiliza sauti wanazoweza kuzisikia darasani.
Katika makundi, au darasa zima likiwa limekuzunguka, wachangie mawazo juu ya sauti zote wanazoweza kusikia kwenye karatasi kubwa au ubaoni. (angalia Nyenzo rejea muhimu: Kutumia ramani za akilini na chemsha bongo kugundua mawazo .)
Baadaye, panga makundi madogo ya wanafunzi (nne/tano) kwenda nje kwa muachano na kutembea kwenye viwanja vya shule. Wasimame katika maeneo manne na kusikiliza kwa makini chochote wanachoweza kusikia. Wachukue kalamu au penseli na vitabu vyao au karatasi kwa ajili hii.
Kila kundi wachukue dondoo kwa kila sauti mpya wanayosikia na mahali walipoisikia, na wajaribu kuainisha ni nini kinatengeneza hizo sauti na kwa namna gani zinatengenezwa.
Wanaporudi darasani, waambie kila kundi wachore ramani zao za kufikirika juu ya sauti walizosikiliza.
Haya yanapoisha, yaonyeshwe ili wote waone na kujadili mawazo yao namna sauti zinavyotengenezwa.
Sehemu ya 4: Kutumia muziki darasani