Somo la 3
Upigaji muziki ni aina ya mawasiliano: vyombo na sauti 'huzungumza', kuwasilisha hisia, mawazo na fikra. Muziki huakisi na kujenga utamaduni, na daima huwa na vuguvugu – linalobadilika na kuendelea. Barani Afrika, muziki ni muhimu kwa kujenga mshikamano wa kijamii (umoja) na unaweza kuwa muhimu darasani.
Katika sehemu hii, utaendeleza vitendo vilivyopita kwa kuandaa maonyesho ya darasa zima. Jinsi ulivyokipanga kitendo ndivyo hivyo kitakavyochangia katika maarifa ya ushirikiano na usikilizaji wa wanafunzi.
Uchunguzi kifani ya 3: Thamani ya kuandaa muziki wa kikundi
Uchu wa Goodluck ni kutengeneza muziki katika kikundi. Hisia anazopata akiwa anapiga marimba, au anapoimba katika kwaya ni maalumu kwa mshikamano. Anataka kuwashirikisha wanafunzi wake hisia hizi; wapate uzoefu wa namna inavyokuwa kutengeneza muziki wa pamoja wakati kila mmoja anamsikiliza mwenzake kwa umakini.
Goodluck anasafiri kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma iliyoko katikati mwa Tanzania, na kutembelea Shule ya Msingi Umoja iliyoko mbalil na mjini. Anamtembelea mwalimu wa sanaa na utamaduni. Anapofika, anakuta kuna sherehe. Makundi ya wavulana wadogo yanapiga filimbi na ngoma wakati wa maandalizi.Kwenye uwanja wa vumbi, Goodluck anasikiliza na kuliona kundi la watoto 50wakisogea na kufanya muziki kwa pamoja-kila mmoja akichangia, akitazama na kusikiliza wanapoeleza hadithi ya ngoma.
Akivutiwa na wapiga filimbi na ngoma, aliamua kuwa wanafunzi wake Dar es Salaam wanahitaji kupata uzoefu wa jinsi gani ilivyo ‘kuwa mmoja’ kwa kutumia muziki. Baada ya kuongea na waalimu na kujifunza zaidi juu ya umuhimu wa muziki kiutamaduni na ngoma ya Mheme, anarudi nyumbani kuandaa somo ambapo wanafunzi wake watatengeneza muziki kwa pamoja.
Nyenzo rejea 6: Kutengeneza muziki inaonyesha ni jinsi gani zana za muziki zinaweza kutengenezwa kwa ajili ya wanafunzi wako kuzitumia.
Shughuli muhimu: Kutengeneza muziki
Waulize wanafunze kama mmoja kati yao anapiga kifaa cha muziki. Kama wanapiga, waambie wavilete shuleni.
Siku inayofuata, waambie wanafunzi walioleta vifaa wavionyeshe na kuvipiga darasani.
Waulize wanafunzi wako kama wanajua nyimbo au mashairi ya majigambo. Kama wanajua, waambie wakuambie maneno, na yaandike ubaoni.
Mwambie mwanafunzi aimbe ushairi/wimbo halafu waambie wanafunzi darasani waungane nawe utakapoimba ushairi/wimbo tena.
Rudia hadi darasa litakapoimba barabara.
Sasa, waambie wale wanaopiga vifaa nao waungane na wenzao. Fanyia mazoezi wimbo mzima hadi kila mmoja atakapofurahi na waimbe kwa darasa lingine au ‘siku ya wazazi’.
Somo la 2: Kufanya kazi katika vikundi ili kutunga ushairi wa wasifu yaani utenzi