Nyenzo rejea 5: Nyimbo za kusifu za mwanafunzi
Taarifa za msingi/welewa wa somo wa mwalimu utangulizi
Gracie – Wimbo wa kusifu
Imba shairi hili na waambie wanafunzi wako wabuni kiitikio kinachoendana na mwito.Chagua vifaa au sauti zinazooana na maneno: juu, iliyojikita, miito, chachu, miongozo na mwezi.
Mwito:
Gracie
Anayeishi kwenye jangwa kuu
Amejikita katika amani
Anaita roho za ngedere na simba Anachachua pamoja na kereng’ende Anaongoza kalamu
Mwezi ukazama
Mstari 1. Gracie (jina langu).
Mstari 2. Anayeishi kwenye jangwa kuu (nilizaliwa na kulelewa hapa
Bend ambalo ni jangwa kuu).
Mstari 3. Amejikita katika amani (babu zangu Mfalme Joseph wa kabila la
Nez Perce alifahamika kwa tabia yake ya amani).
Mstari 4. Anaita roho za ngedere na simba (wanyama wangu wanaowakilisha mizimu ni ngedere na simba. Ngedere huonyesha hulka yangu ya utotoni na simba huonyesha nguvu, ufahari na ukatili).
Mstari 5. Anachachua pamoja na kereng’ende (Kereng’ende anawakilisha mawazo yangu, mapenzi na ndoto).
Mstari 6. Anaongoza kalamu (Napenda kuchora na haya ni mapenzi yangu).
Mstari 7. Mwezi ukazama (Wakati wa usiku ndipo ninapopata faraja, nyota hunipa matumaini na mwezi ndio naweza kuuamini katika matatizo yangu).
Kuandaa shairi la kusifu au wimbo (maelekezo kwa mwanafunzi)
Anza na jina lako.
Rejea kwenye kitu kinachoelezea wapi na namna ulivyozaliwa
Ongea kitu chochote juu ya urithi wa familia yako;asili ya familia yako. Taja kitu, mnyama, kitu asilia ambacho ni cha maana au maalumu
kwako.
Ongea kitu kukuhusu wewe: unapenda nini, unataka nini na ndoto zako.
Andaa shairi kati ya mistari mitano na minane. Shairi liwe fupi, kila neno libebe picha, (kila neno liwe na maana nyingi, likitueleza mambo mengi).
Chagua maneno yako kwa uangalifu. Tumia kifaa chako kuboresha hisia na maana ya shairi lako. Chagua lini na ni vipi utaitengeneza sauti. Fikiri kwa makini kuhusu namna utakavyotumia sauti yako kujieleza.
Unaweza kuona zaidi nyimbo za kusifu za mwanafunzi katika tovuti ifuatayo: http://web.cocc.edu/ catagucci/ [Tip: hold Ctrl and click a link to open it in a new tab. (Hide tip)] ambako yaliyopo hapo ya juu ndiko yalikonakiliwa.
Nyenzo rejea 4: Kusifu uimbaji