Nyenzo rejea 6: Kutengeneza muziki

Taarifa za msingi/welewa wa somo wa mwalimu utangulizi

A. Kutengeneza na kupiga filimbi za Tshikona

Kutengeneza kundi la wapiga filimbi

(kutoka Talking Drum, April 1999, Sandra Bonnett, p. 17–18)

Wapiga filimbi ni makundi maalumu ya muziki kwa sababu kila mtu anapiga nota moja tu-lakini, zinawekwa pamoja, mara nyingi katika njia za kutatanisha, zinatengeneza muziki wa kustaajabisha. Wavha Venda, Watswana na Wabapedi wanafahamika kwa makundi yao ya wapiga filimbi za mitete, ambazo zinasemekana kwenda sambamba na ngoma kama Venda Tshikona na Bapedi Dinaka. Filimbi zimetengenezwa kwa matete (sehemu za vijijini) au filimbi za chuma (sehemu za mijini au kwenye machimbo ya madini). Filimbi zinatofautiana kwa ukubwa kutoka

sentimeta 20 hadi mita moja kwa urefu, ikitoa nota kuanzia za juu hadi za chini.

Shughuli hii imeelemea kwenye muziki kiTshikona na filimbi iliyochezwa na Wavenda wanaoishi kaskazini kabisa mwa Afrika ya Kusini (Jimbo la Limpopo). Filimbi za kiTshikona ni ndefu zikiwa na urefu wa kutofautiana, kila moja ikitoa nota tofauti. Unaweza kutengeneza filimbi zako kwa kutuma mabomba ya plastiki kama vile yale ya kupitishia nyaya za umeme, vipande vya mabomba ya plastiki, mabomba ya umwagiliaji (kipenyo cha mm 12-15). Tengeneza filimbi za urefu uliotofautiana ili uwe na nota tofauti. Vile vile ungeweza kutumia chupa za ukubwa mbalimbali na kupuliza kwa juu ili kutoa sauti.

Jinsi ya kupiga filimbi

1.     Weka sehemu ya wazi ya kifaa kwenye midomo ya chini.

2.     Shikilia filimbi kati ya vidole vyako, kidole cha shahada na kidole gumba.

3.     Weka vidole vilivyobaki kuzunguka eneo la katikati la kifaa.

4.     Anza kupuliza taratibu juu ya shimo hadi hapo nota itakapotokea.

5.     Jaribisha kwa kuziba sehemu ya chini ya filimbi kwa mkono wako.

B. Kutengeneza muziki wa kidemokrasia

Wagawe wanafunzi katika makundi ya watu kumi na jaribisha filimbi za mitete, ili waweze kusikilizana kwa umakini. Tengeneza nafasi katika mapigo yako ili wanafunzi waweze kujaza nafasi hizo. Halafu ongeza na mbinu za kucheza. Huna haja ya kucheza muda wote. Pokezaneni.

Unganisha- kujaza nafasi

Wazo la kuunganisha ni la msingi kwa muziki wa kiafrika. Unapojiunganisha na sauti unakuwa unajaza nafasi katika muziki (ukimya) kwa kutumia sauti. Kwa maneno mengine unasubiri hadi upate

nafasi ya kutoa sauti yako. Huu ni ujuzi muhimu unaofundisha wajifunzaji kusikiliza kwa makini, achianeni na kuweni makini. Huu ni msingi wa kutengeneza muziki wa kikundi kama picha za sauti.

C. Kutumia chupa kutengeneza filimbi za muziki wa makundi.

Kama ulitengeneza chupa za muziki badala ya filimbi, zituni chupa zako ili kuwe na namba sawa ya chupa zilizokuwa zimewekwa kwenye sauti A, E, G and D (kuanzia ya juu hadi ya chini). Utahitaji kitunio au kinanda ili kukagua tuni zako na kurekebisha maji kwenye chupa yako.

Wagawe wanafunzi wako katika makundi mawili. Hapa kuna mpangilio wa muziki kwa kila kundi uliogawanywa katika mapigo 8. Jaribisha kwanza kwa kupiga makofi kwenye namba zilizokolezwa wino, wakati mtu mwingine akipiga ngoma ya besi kuhifadhi mapigo. Utunze huo mdundo wa ngoma katika hali yake ya taratibu. Halafu puliza kwenye chupa yako katika muda sahihi, ukitunza mapigo kwa kutumia ngoma (lazima ujue ni nota gain ngoma yako inasikika!)

Kundi A

Chupa zote za A katika kundi la ‘lahani’ zinapuliza kwenye namba 1 na 5;

chupa zote za G zinapuliza kwenye namba 2 na 6, n.k.

Kundi A

Hesabu/Idadi ya nota

A12345678
G12345678
E12345678
D12345678

Kundi B

Hesabu/Idadi ya nota

A12345678
E12345678
D12345678

Weka makundi yote mawili pamoja, sikiliza kwa umakini kwenye ngoma ili ujue ni mdundo gani wa kupiga. Muziki utakaopatikana unatakiwa uwe wa kuvutia. Ukishafanyia mazoezi, tengeneza muziki wako, kwa kucheza nota hizo kwa mapigo tofauti.

(Kazi ya Sandra Bonnett, 1997. In Talking Drum April 1999)

D. Nyenzo katika jamii na bendi

Kwa ajili ya mwalimu:

Endelezeni mradi huu kwa kuunda kabendi, kwa kutumia vifaa vilivyotengenezwa na wanafunzi. Hakikisha kuwa kila kundi lina vifaa kadhaa. Jenga dhamira ya utambulisho wa kundi na aina ya nyimbo za kusifu ili kila kundi litengeneze shairi kwa kutumia vifaa, ikiwasilisha jambo kuwahusu wao wenyewe. Kutengeneza nyimbo za makundi kunahitaji muda kama mchakato wa kujifunza namna ya kutengeneza muziki kwa pamoja unavyojengeka. Shirikiana pamoja na mwalimu na shule yako rafiki. Andaa mchezo wa pamoja ambapo kila kundi linacheza nyimbo zake na kuonyesha vifaa walivyotengeneza.

Tafuta nini kinatokea kimuziki katika jamii yako. Kunaweza kuwa na wanamuziki wazuri ambao wangeweza kuja na kuimba kwa wanafunzi wako, na kushiriki nao katika shughuli za muziki na utamaduni. Tumia jamii kama nyenzo ya kujifunzia.

Kwa ajili ya wanafunzi: Mawazo ya mradi wa utafiti

Tafuta mwanamuziki anayeishi kaitka eneo lako na umhoji. Muulize:

Kifaa chako ni nini?

Ni aina gani ya muziki unaimba?

Muziki unamaanisha nini kwenye maisha yako? Wapi na vipi ulijifunza kuimba?

Tafiti aina mbalimbali za makundi ya muziki: kwaya, bendi, muziki wa pop/rock/kizazikipya/ngoma za asili na aina nyingine ya makundi.

Tafuta:

Ni nini kinachofanya kila kwaya au bendi iwe ya kipekee? Wanacheza muziki gani?

Wanatumia vifaa gani?

Muziki wao umerekodiwa? Kama ndiyo walirekodi vipi?

Ni akina nani waliohusika katika kutoa wimbo au albamu iliyorekodiwa? Wanafanya nini?

Ni hatua gani muhimu za kuchukua ili kuunda kundi la muziki lenye mafanikio?

Mazoezi ya mwisho yanafanyaje kazi?Ni namna gani kikundi au kwaya inafanya mazoezi?Wapi?Kwa muda gani?

Ni namna gani bendi au kwaya inavyojiimarisha yenyewe na matamasha yao?

Kutengeneza bendi yangu mwenyewe

Kwa kutumia taarifa ambazo umekusanya unda kundi na baadhi ya rafiki zako na tumia vifaa vyako kutengeneza kibendi chako mwenyewe. Ipe bendi hiyo jina. Fikiri kuhusu aina ya muziki ambao ungependa kuucheza. Tengeneza sauti zako mwenyewe. Endelea kubuni vifaa. Endelea kusikiliza na kugundua sauti za kuvutia ambazo unaweza kutengeneza na ziweke pamoja ili utengeneze muziki wako mwenyewe.

Kuona jinsi wanafunzi wengine walivyounda vibendi vyao, nenda www.soundhouse.co.uk/ mixedup/ [Kidokezo: shikilia Ctrl na ubofye ili uifungue katika kichupo kipya (Ficha kidokezo)]

Nyenzo rejea 5: Nyimbo za kusifu za mwanafunzi

Sehemu ya 5: Sanaa ya kuhadithia hadithi