4.8.2 Visababishi vya tatizo la fetasi

Hali nyingi huathiri afya ya fetasi wakati wa leba na wa kuzaa. Lazima fetasi iwe na plasenta inayofanya kazi vizuri na virutubisho na oksijeni kutoka kwa damu ya mama mjamzito. Ulijifunza jambo hili katika Kipindi cha 5 cha Somo ya Moduli ya Utunzaji katika ujauzito. Ikiwa damu ya mama au plasenta haifanyi kazi vizuri, fetasi yuko katika hatari ya asifiksia. Fetasi aliye na asifiksia huwa na mpigo wa moyo ulio wa kiwango kilicho mbali na ya kawaida. Hali nyingine zinazoweza kuathiroi afya ya fetasi zinaweza kuonyeshwa na kiwango cha mpigo wa moyo usiokuwa sawa. Hali hizi zimeonyeshwa katika Kisanduku 4.1.

Ulijifunza kuhusu hitilafu za shinikizo la damu wakati wa mimba, anemia ya wajawazito, na kuachilia kwa plasenta katika Vikao vya 18, 19, na 21 vya Somo la Moduli ya Utunzaji katika ujauzito, Sehemu ya 2.

Kisanduku 4.1 Sababu zinazopelekea mpigo wa moyo wa fetasi kutokuwa wa kawaida

Damu kutoka kwa plasenta hadi kwa fetasi hupungua, hali inayotokea mambo haya yanapofanyika:

  • Hitilafu ya shinikizo la damu katika ujauzito.
  • Mama akiwa na anemia.
  • Upungufu wa kiasi cha damu ya mama, ambayo huwa ni haipovolemia. Hutokea kutokana na upungufu wa damu, au upungufu wa viowevu mwilini kupitia kutapika na kuhara.
  • Haipoksia ya mama, ambayo ni ukosefu wa oksijeni. Hutokea mama akiwa na ugonjwa wa moyo au wa mapafu, au akiishi katika mwinuko wa juu sana.
  • Plasenta iliyo "nzee."
  • Amnioni inakuwa kiasi kidogo, na kuzuia fetasi kusonga kwa urahisi. Mwili wa mtoto unaweza kufinya kambakitovu kwa ukuta wa uterasi.
  • Kambakitovu inafinywa. Hutokea ikija chini ya njia ya uzazi kabla ya fetasi, au ikizunguka shingoni mwa mtoto.
  • Plasenta ikitengana na ukuta wa uteresi mapema, ambayo ni kuachilia kwa plasenta.

Hesabu kiwango cha mpigo wa moyo wa fetasi kila dakika 30 na uweke alama kwenye patografu. Patografu inaweza kusaidia kugundua mkwepuko wowote mbali na ya kawaida. Ukigundua kiwango cha mpigo wa moyo wa fetasi wowote usio wa kawaida, usisubiri dakika 30 zingine. Pima kiwango cha mpigo wa moyo wa fetasi mara nyingi iwezekanavyo. Iwapo huo mpigo usio wa kiwango cha kawaida utaendelea kwa zaidi ya dakika 10, mpe mama aliye katika leba rufaa haraka.

4.8.1 Kiwango cha mpigo wa moyo wa fetasi kama daliliya tatizo la fetasi

4.8.3 Nakili kiwango cha mpigo wa moyo wa fetasi kwenye patografu