4.8.4 Amnioni kama dalili ya tatizo la fetasi

Dalili nyingine ya tatizo la fetasi ambayo tayari imetajwa ni amnioni iliyo na mekoniamu (rangi ya kijani au amnioni nyeusi). Amnioni iliyo na mekoniamu kidogo sio lazima iwe ni ishara ya shida kwa fetasi, isipokuwa iwe pamoja na uendelevu wa mabadiliko ya kiwango cha mpigo wa moyo wa fetasi usio wa kawaida.

Uchunguzi ufuatao hufanywa wakati wa kila kipimo cha uke na kunakiliwa kwenye patografu, chini baada tu ya pahali kiwango cha mpigo wa moyo wa fetasi ulionakiliwa.

Ikiwa membreni ya fetasi haijapasuka, andika herufi 'I' ('iliyo kamilika’).

Iwapo membreni imepasuka na:

  • Hakuna amnioni, andika 'A' (ikiwa 'hakuna')
  • Amnioni ni dhahiri, andika 'C' (ikiwa ni'dhahiri')
  • Amnioni ina damu, nakili 'B'
  • Amnioni ina mekoniumu, rekodi 'M1' ikiwa kidogo, 'M2' ikiwa nene kidogo na 'M3' kwa amnioni nzito sana iliyo kama supu (Kisanduku 4.2).

Jedwali 4.2 Kadiri ya kiasi cha mekoniamu

Mpe mama aliye katika leba rufaa kwa kituo cha afya cha gazi ya juu mapema iwezekanavyo ukiona mambo haya:

  • Amnioni M1 katika kipindi cha kwanza cha leba kwa awamu fiche, hata ikiwa kiwango cha mpigo wa moyo wa fetasi uko kawaida.
  • Amnioni M2 katika kipindi cha kwanza cha leba kwa awamu iliyo imarika, hata ikiwa kiwango cha mpigo wa moyo wa fetasi ni cha kawaida.
  • Amnioni M3 katika kipindi chochote cha leba, isipokuwa leba ikiendelea haraka.

4.8.3 Nakili kiwango cha mpigo wa moyo wa fetasi kwenye patografu

4.9 Tathmini hali ya afya ya mama