Swali la Kujitathmini la Kipindi cha 4

Sasa kwa kuwa umekamilisha Kipindi hiki cha somo, jibu maswali haya kutathmini uliyojifunza. Unaweza kuangalia majibu yako kwenye vidokezo kuhusu Swali la Kujitathmini vilivyo mwishoni mwa Moduli ya huduma ya leba na kuzaa.

Soma Uchunguzi Kifani 4.1 na ujibu maswali.

Uchunguzi maalum 4.1 Kisa cha Bekelech

Bekelech ni mama mwenye gravida5 na para4. Mimba ya sasa imefikia umri wa ujauzito wa wiki 40 na siku 4. Unapofika kwa nyumba yake, unampata akiwa katika leba.Wakati wa utathmini wako wa kwanza, alikuwa na mikazo ya uterusi 4 kila dakika 10, kila moja ikidumu kwa sekunde 35-40. Ulipima uke wake na kichwa cha fetasi kilikuwa katika alama ya -3 na seviksi ilikuwa imepanuka sentimita 5. Mpigo wa moyo wa fetasi ilihesabiwa kuwa midundo 144 kwa dakika.

Maswali ya Kujitathmini 4.1 (Malengo ya Somo la 4.1, 4.2, na 4.3)

 1. Ina maana gani kusema Bekelech ni mama mwenye ‘gravida 5 na para 4’?
 2. Unawezaje kueleza umri wa ujauzito wa mtoto?
 3. Amefika kipindi gani cha leba na kichwa cha mtoto kimeingia kwenye pelvisi?
 4. Mpigo wa moyo wa fetasi kiwango cha kawaida au la?
 5. Ungefanya nini ili kufuatilia mwendeleo wa leba hii?
 6. Ni mara gapi ungepima uke wa Bekelech na kwa nini?

Answer

 1. Kama mama gravida 5, para 4, Bekelech amekuwa na mimba 5 na moja haikuzaliwa ikiwa hai.
 2. Kwa wiki 40 na siku 4, mimba imetimiza muda wa kuzaliwa.
 3. Seviksi ya Bekelech imepanuka sentimita 5 na ana mikazo ya uterusi 4 kila dakika 10 kila moja inadumu sekunde 35-40. Bekelech ameingia katika kipindi cha kwanza cha awamu ya leba iliyoimarika. Katika alama ya -3, Kichwa cha fetasi bado hakijateremka kwa pelvisi.
 4. Mpigo wa moyo wa fetasi uko kwa kiwango cha kawaida kati ya midudo 120-160 kwa dakika.
 5. Leba iko katika awamu iliyoimarika na seviksi imepanuka zaidi ya sentimita 4. Una fuatilia kwa utaratibu mwendeleo wa leba yake mara moja, ishara zake muhimu na viashiria vya tatizo la fetasi. Andika vipimo hivi kwenye patografu (Mchoro 4.1 na Sehemu 4.2.1)
 6. Unaamua kupima uke wake mara nyingi zaidi kuliko saa 4 za kawaida. Leba hii inaweza kuendelea haraka kwa sababu Bekelech ni mama aliye multigravida na multipara. Kuwa mwangalifu kwa ishara za matatizo yoyote, kwa sababu Bekelech tayari alipoteza mtoto mmoja kabla ya kuzaliwa.

Mwisho wa jibu

Maswaliya Kujitathmini 4.2 (Malengo ya Somo la 4.2)

Toa sababu mbili za kutumia patografu

Answer

Tumia patografu kwa sababu hizi mbili muhimu:

 1. Ikitumika kwa usahihi, inaweza kukusaidia kutambua leba ikiendelea kwa kawaida, na ikiwa lazima umpe mama rufaa ya hospitali. Leba ikiendelea vizuri, habari iliyo kwenye patografu inakuonyesha wewe na mama kwamba yeye na mtoto wake wako katika afya nzuri.
 2. Utafiti umeonyesha kwamba matatizo katika fetasi wakati wa leba ya muda mrefu ziko chini wakati mhudumu wa kuzalisha anapotumia patografu kufuatilia mwendeleo wa leba.

Mwisho wa jibu

Maswaliya Kujitathmini 4.3 (Malengo ya Somo la 4.1, 4.3, 4.4 na 4.5)

 1. Ni viashiria vipi vya mwendeleo mzuri wa leba utaonakili kwenye patografu?
 2. Ni viashiria vipi vya afya bora ya fetasi utakaonakili kwenye patografu?
 3. Ni kwa mara ngapi utapima ishara muhimu za mama na kunakili kwenye patografu wakati wa leba inayoendelea vizuri?
 4. Ni viashiria vipi kuu vya kuhitaji rufaa kwa mara moja?

Answer

1. Mwendeleo mzuri wa leba unaonyeshwa na mambo haya:

 • wakati seviksi inapopanuka kwa kiwango sawa au upande wa kushoto wa mstari wa Tahadhari kwenye patografu
 • ushahidi kuwa fetasi anateremka vile seviksi inatanuka
 • mikazo ya uterasi zinazoendelea kuongezeka kwa muda na idadi kila dakika 10

2. Hali ya afya bora kwa fetasi inaonyeshwa na mambo haya:

 • mpigo wa moyo wa fetasi wa kiwango cha midundo kati ya 120-160 kwa dakika (isipokuwa tofauti kidogo inayodumu chini ya dakika 10)
 • ufinyanzi (upishani wa mifupa ya kichwa ya fetasi) usiyo zidi +2
 • amnioni nyeupe au iliyobadilika kidogo (C au M1)

3. Wakati wa leba inayoendelea vizuri, pima vitu hivi vya mama na uviandike kwenye patografu:

 • shinikizo la damu (kila baada ya saa 4)
 • mdundo wa moyo (kila baada ya dakika 30)
 • joto (kila baada ya saa 2
 • mkojo (kila anapokojoa)

4. Toa rufaa mara moja utakapoona moja kati ya vitu hivi:

 • upanuzi wa seviksi wa polepole ( kwa upande wa kulia wa mstari wa Tahadhari kwenye patografu)
 • mwendeleo duni wa leba kukiwa na ufinyanzi wa kichwa cha fetasi wa +3
 • kiwango cha mpigo wa moyo wa fetasi ukiendelea kuwa chini ya midudo 120 au zaidi ya 160 kwa dakika
 • amnioni ilio na mekoniamu, ikitegemea kipindi cha leba, hata ikiwa mpigo wa moyo wa fetasi uko kwa kiwango cha kawaida. Toa rufaa ukiona :
  • Amnioni M1 wakati wa kipindi cha kwanza cha awamu ya leba fishe
  • Amnioni M2 wakati wa mwanzo wa kipindi cha kwanza cha awamu ya leba ilio imarika
  • Amnioni M3 wakati wowote wa leba isipokuwa leba ikiendelea haraka Mwisho wa jibu

Muhtasari wa Kipindi cha 4