4.2 Sehemu za patografu

Patografu ni chati yako ya mama aliye katika leba (Mchoro 4.1). Juu ya chati, andika jina na umri wa mama na hali ya "gravida" na "para". Andika kituo chake cha afya au nambari yake ya usajili ya hospitali. Andika tarehe na saa uliyoanza kumhudumia wakati wa kuzaa. Andika wakati membreni za fetasi zilipopasuka.

  • Je, kuna tofauti gani kati ya mwanamke ambaye ni multigravida na yule ambaye ni multipara?

  • Multigravida ni mwanamke ambaye amepata mimba angalau mara moja kabla ya mimba iliyoko. Multipara ni mwanamke ambaye amezaa hapo awali watoto walio na uhai angalau mara mbili kabla ya sasa.

    Mwisho wa jibu

Iwapo utatumia chati nyingine, unaweza kuandika taarifa zingine nyuma ya patografu. Andika historia ya uzazi ya mwanamke na ya matibabu aliyoyapata pamoja na ya sasa. Andika taarifa kutokana na ukaguzi wa mwili na hatua zozote ulizoanzisha. (Pamoja na dawa, maelezo ya kuzaa, na rufaa.)

4.1 Kwa nini patografu ni muhimu

4.2.1 Sehemu za grafu ya patografu