4.3 Nakili na ueleze maendeleo ya leba

Wakati wa leba inayoendelea kwa kawaida, seviksi hupanuka angalau sentimita 1 kwa saa moja wakati leba imeingia hatua ya kwanza iliyoimarika. Utajifunza taarifa hii katika Kipindi cha 1 cha Somo.

Isipokuwa ukigundua matatizo kwa mama au fetasi, hesabu mpigo wa moyo wa fetasi kila dakika 30 kwa dakika moja kamili. Hesabu mkazo wa uterusi kwa dakika 10.

Mwanzo, pima uke kutathmini mambo haya:

  • Kiwango cha sevikisi kupatana na kichwa cha fetasi (Rejelea mchoro 1.1) na upanuzi wa seviksi
  • Sehemu ya fetasi inayotangulia
  • Hali ya membreni ya fetasi (imeshikana au imepasuka ) na amnioni
  • Ukubwa wa pelvisi ya mama ili kubaini kama ukingo ni mkubwa kutosha motto kupita.

Kisha baada ya, kila saa 4, angalia mabadiliko katika mambo haya:

  • Upanuzi wa seviksi
  • Ukuaji wa edema kwa seviksi. (Seviksi nyembamba inaweza kuvimba ikiwa mama ataanza kumsukuma mapema zaidi. Seviksi inaweza kuvimba ikiwa leba itachukua muda mrefu na seviksi haijatanuka sana.)
  • Kama unaweza kutambua hali ya fetasi,
  • Namna kichwa cha fetasi kimeteremka
  • Ukuaji wa ufinyanzi na kaputi (Kipindi cha 2)
  • Rangi ya amnioni (ikiwa membreni ya fetasi tayari imepasuka).

Andika matokeo ya uchunguzi wako kwa patografu kwa vipindi vilivyopendekezwa wakati leba inapoendelea. Alama zinakuonyesha kama kila kitu kinaendelea vizuri au ikiwa vipimo vinasababisha wasiwasi. Unapoandika kwa patografu, hakikisha unafanya mambo haya:

  • Tumia fomumoja ya patografu kwa kila mama aliye katika leba. (Unaweza kufikiri kuwa leba ya ukweli imeanza na uandike kwa patografu, lakini baadaye utambue kwamba ilikuwa bandia. Unaweza kumtuma mama nyumbani au umshauri kuendelea na shughuli zake za kawaida za kila siku. Wakati leba umedhibitishwa, tumia patografu mpya).
  • Andika kwenye patografu wakati leba iko katika hatua ya kwanza iliyoimarika (Seviksi imetanuka sentimita 4 na juu zaidi).
  • Andika wazi, ili kila anayefahamu kuhusu patografu anaweza kuelewa na kueleza alama zako.
  • Kama ni lazima umpatie mama rufaa kwa kituo cha afya cha ngazi ya juu, tuma patografu na barua yako ya rufaa. Andika maelezeo yako ya patografu katika hiyo barua.
  • Bila kurejelea sehemu za awali, andika kwa haraka vipimo vya patografu vilivyo lazima ili kufuatilia miendo ya leba.

  • Linganisha orodha yako na patografu katika mchoro 4.1. Kama huna uhakika hata kidogo kuhusu vipimo vyovyote, basi soma tena Sehemu za 4.2 na 4.3.

    Mwisho wa jibu

4.2.2 Mistari ya Tahadhari na Hatua

4.4 Kupanuka kwa seviksi