4.4 Kupanuka kwa seviksi

Kama ulivyo soma katika Kipindi cha 1, hatua ya kwanza ya leba imegawanywa katika awamu iliyofishe na ya leba iliyoimarika. Awamu fishe hudumu hadi seviksi itanuke sentimita 4 na iwe imepatana na kichwa cha fetasi (Mchoro 1.1). Awamu fishe hudumu hadi saa 8, ingawa kwa kawaida huwa fupi zaidi. Tathmini afya ya mama na fetasi na uandike matokeo yote. Hata hivyo, usiandike habari hii kwa patografu hadi leba iimarike.

Kipimo cha ukeni hufanywa kwa takriban kila baada ya saa 4 hadi mtoto azaliwe. Awamu iliyomarika huanza wakati seviksi hupanuka sentimita 4. Awamu iliyoimarika hukamilika wakati upanuzi umekamilika, yaani, sentimita 10. Seviksi hupanuka sentimita 1 kwa saa moja wakati wa awamu iliyoimarika. (Seviksi utapanuka upesi katika akina mama waliowahi kuwa wajawazito mara mbili au zaidi).

Katika sehemu ya upanuzi wa seviksi kwa patografu, chini upande wa kushoto, kuna nambari 0-10. Kila namba/mraba inawakilisha upanuzi wa sentimita 1. Chini ya sehemu hii kuna miraba 24, kila moja inawakilisha saa 1. Baada ya kila saa 4, pima uke na ukadirie jinsi seviksi inatanuka. Andika alama X kwa patografu kwa nambari hiyo. Angalia seviksi ya wanawake waliowahi kuzaa mara mmoja au zaidi mara nyingi zaidi kuliko kila baada ya saa 4 wakati leba umeimarika zaidi. Mara nyingi wao huendelea haraka kuliko wanawake ambao wanazaa kwa mara ya kwanza.

  • Kwa mfano katika mchoro 4.2, ni tofauti gani katika upanuzi wa seviksi imerekodiwa kwa kipindi na muda gani?

    Mchoro 4.2 Mfano wa jinsi ya kunakili upanuzi wa seviksi (zilizoandikwa na alama za X) na kuteremka kwa kichwa cha fetasi (zilizoandikwa na alama za 0) kwa patografu.
  • Seviksi ilikuwa imepanuka sentimita 5 saa 1 baada ya kuanza ufuatiliaji wa uchunguzi wa kuzaa. Baada ya saa zingine 4, seviksi ya mama ilikuwa imepanuka kikamilifu sentimita10.

    Mwisho wa jibu

Kama uchunguzi wa kuzaa kutaendelea vizuri, alama ya upanuzi wa seviksi hubaki juu au upande wa kushoto wa mstari wa Tahadhari.

Ikiwa membreni imepasuka na mama hana leba, usipime uke kwa vidole. Huwezi kutambua leba na unaweza kuanzisha maambukizi. (Kupasuka kwa mapema wa membreni, umeelezwa katika Kipindi 17 cha Somo la Moduli ya Utunzaji katika Ujauzito)

4.3 Nakili na ueleze maendeleo ya leba

4.5 Kushuka kwa kichwa cha fetasi