4.5 Kushuka kwa kichwa cha fetasi

Leba kunapoendelea vizuri, kichwa cha fetasi hushuka kadiri seviksi inavyopanuka. Andika kushuka huko kwa sehemu hiyo ya patografu, lakini tumia O kama ishara. Kukadiria maendeleo ya kushuka kwa fetasi, tathmini pahali kichwa cha fetasi kimefika kwenye pelvisi (Mchoro 4.3). Pima uke kwa vidole vilivyo na glavu. Hisi sehemu inayotangulia kwa fuvu ya fetasi ukilinganisha na sehemu nyembamba ya mfupa wa iskiamu katika ukingo wa pelvisi ya mama.

Mchoro 4.3 Tathmini pahali pa kichwa cha fetasi kwa kupima uke, ukilinganisha na sehemu nyembamba ya mfupa wa iskiamu katika ukingo wa pelvisi ya mama. (Chanzo: Shirika la Afya Duniani, 2008, Midwifery Education Module: Managing Prolonged and Obstructed Labour, Mchoro 7.28, ukurasa 132)

Mchoro 4.3 kinaonyesha kuwa stesheni 0 ni wakati kichwa cha fetasi kiko katika kiwango kimoja na sehemu nyembamba ya mfupa wa iskiumu. Iwapo kichwa kiko juu ya njia ya uzazi kupita sehemu nyembamba ya mfupa wa iskiumu, alama hupewa nambari ya kutoa. Katika alama -4 au -3 kichwa cha fetasi bado kina "elea" na hakijaingia kwenye pelvisi. Katika alama ya -2 au -1, kichwa kiko karibu na sehemu nyembamba ya mfupa wa iskiamu.

Iwapo kichwa cha fetasi kiko chini ya njia ya uzazi kupita sehemu nyembamba ya mfupa wa iskiamu, alama hupewa nambari ya kuongeza. Katika amala +1 na hata zaidi katika alama +2, sehemu ya kichwa cha mtoto huwa hutoka wakati wa mikazo. Katika alama ya +3, kichwa kinatokea kwa uke ya mama, kumaanisha kinaonekana katika ufunguzi wa uke hata kati ya mikazo. Seviksi sasa inapaswa kuwa imepanuka kikamilifu.

Ni tatizo kuweka alama mbalimbali ya uteremkaji wa fetasi kwa patografu. Alama ya upanuzi wa seviksi na kushuka chini kwa kichwa huwa na kipimo cha 0-10 katika mizani. Kwa kawaida, thamani ya 0 hadi 5 hutumiwa kunakili kiwango cha kushuka chini kwa fetasi. Jedwali 4.1 linaoonyesha jinsi ya kubadilisha alama ya kichwa cha fetasi (Mchoro 4.3) ili kuweka alama kwa patografu kwa kuandika O. (Kumbuka, kuweka alama ya kwenda chini kwa fetasi na alama za O na upanuzi wa seviksi na alama za X, ili zote mbili hazichanganywe).

Kichwa cha mtoto kinapotokea kwa uke ya mama (alama ya +3), unaweza kukosa wakati wa kuandika O kwenye patografu!

Jedwali 4.1 Alama ya kichwa cha fetasi (inayoamuliwa na kupima uke) na alama ya kushuka kwa fetasi kwa patografu.
Alama ya kichwa cha fetasi (Mchoro 4.3)Alama kwa patografu
–4 or –35
–2 or –14
03
+12
+21
+30
  • Nini maana ya crowning na inakueleza nini?

  • Crowning inamaanisha kwamba sehemu inayotangulia kwa fuvu ya fetasi inaonekana kati ya mikazo. Wakati kichwa cha mtoto kinapotokea kwa uke wa mama, seviksi inatanuka kikamilifu.

    Mwisho wa jibu

4.4 Kupanuka kwa seviksi

4.6 Tathmini ufinyanzi na utengenezaji wa kaputi