6.1.1 Taratibu za asilia katika awamu ya tatu ya leba
Katika leba ya kawaida, awamu ya tatu ni wakati taratibu asilia za kifisiolojia huusababisha kutolewa kwa ghafla kwa plasenta na membreni za fetasi. Ni sharti seviksi ibakie wazi na uterasi kukazana vyema ili mama asikumbwe na matatizo. Katika kauli nyingi, taratibu hizi hutokea katika mfululizo ufuatao.
- Kutengeka kwa plasenta:Plasenta hutengana na pembeni mwa uterasi (Mchoro 6.1a na b)Plasenta inapobambuka, damu iliyo ndani ya vishipa vidogo kwenye mzizi wa plasenta huanza kugandia katikati mwa plasenta na misuli ya pembezoni mwa uterasi. (Pembezo hii ya uterasi hujulikana kama miometriamu).
- Kushuka kwa plasenta:Baada ya kutengeka, plasenta hushukia chini ya njia ya uzazi hadi kupitia seviksi iliyopanuka (Mchoro 6.1c).
- Kutolewa kwa plasenta:Plasenta hutolewa kabisa kutoka kwenye njia ya uzazi (Mchoro 6.1d).
Utaratibu huu wa kutolewa kwa plasenta huashiria awamu ya tatu ya leba. Misuli ya uterasi huendelea kukazana kwa kishindo hivyo kuigandamiza mishipa ya damu iliyochibuka. Tuko hili pamoja na kuganda kwa damu husitisha kuvuja kwa damu baada ya kuzaa.
6.1 Awamu ya tatu ya leba