6.1.2 Matatizo katika awamu ya tatu ya leba

Kipindi cha 11 kinaelezea kwa kina kuhusu kuvuja kwa damu baada ya kuzaa na uterasi isiyo na mikazo. Istilahi zingine zilizo kwenye Kisanduku 6.1 zimeelezwa katika kipindi hiki.

Wanawake wanaozaa bila usaidizi wa mhudumu wa afya aliyehitimu wako katika hatari kuu zaidi ya kukumbwa na matatizo katika awamu zote za leba. Kisanduku 6.1 kinaorodhesha matatizo yanayoweza kutokea katika awamu ya tatu. Matatizo yanaweza kutokea hata wakati plasenta imepandikika vyema katika sehemu ya 2/3 ya uterasi. Matatizo yanaweza kutokea wakati leba haijaendelea kwa muda mrefu na wakati utaratibu wa kuzaa ni wa kawaida. Katika leba ya kawaida, plasenta inatarajiwa kutolewa kwa utaratibu wa kawaida na unaojianzisha wenyewe katika awamu ya tatu ya leba. Hata hivyo, matatizo yanaweza kutokea. Jiweke tayari kwa jambo lolote la dharura lisilotarajiwa.

Kisanduku 6.1 Matatizo yanayotokea mara nyingi katika awamu ya tatu ya leba

Matatizo yafuatayo yanaweza kutokea iwapo hutatumia utaratibu wa UTATL kudhibiti awamu ya tatu.

Plasenta iliyosalia

Plasenta inasalia ndani ya uterasi kwa zaidi ya dakika 30 baada ya mtoto kuzaliwa. Plasenta husalia kufuatia sababu zifuatazo:

  • Mikazo ya uterasi ni hafifu sana, hivi kwamba haisukumi plasenta nje.
  • Seviksi ilirejea upesi sana huku ikifungika nusu. Plasenta imekwama ndani ya uterasi.
  • Kibofu kimejaa hivyo kuzuia kutolewa kwa plasenta.

Kuvuja damu kwa wingi

Kuvuja damu baada ya kuzaa ni hali ambapo mama anavuja zaidi ya mililita 500 za damu baada ya kuzaa. Damu nyingi huvujia katika sehemu ambapo plasenta ilikuwa imeshikamana na uterasi. Damu ni ng’avu au nzito na yenye kunata. Damu nyingi huvuja iwapo uterasi haikazani ifaavyo, hasa kufuatia sababu hizi:

  • Plasenta iliyotengeka nusu huku ikibaki imejipandikiza kwenye pembezo mwa uterasi.
  • Plasenta iliyotengeka kabisa lakini inayosalia ndani ya uterasi.
  • Uterasi isiyo na mikazoMisuli ya pembezo mwa uterasi haikazani kwa nguvu za kutosha kusitisha damu kuvuja baada ya plasenta kutengeka.

Kugeuka kwa uterasi

Sehemu ya ndani ya uterasi huvutika hadi kuja juu mtoto au plasenta inapotolewa. Sehemu ndogo ya uterasi hutokezea ukeni.

6.1.1 Taratibu za asilia katika awamu ya tatu ya leba

6.2 Udhibiti tendeti katika hatua ya tatu ya leba (UTATL)