6.3 Usaidizi katika matatizo baada ya kutumia UTATL
6.3.1 Kuvuja damu kwa wingi
Katika Kipindi cha 11, utajifunza fasili ya kuvuja damu kwa wingi na hatua unazofaa kuchukua iwapo mwanamme anavuja damu baada ya kuzaa. Kipindi cha 11 pia kinaeleza hatua za kuingilia kati ambazo zinafaa kuchukuliwa katika awamu ya tatu ya leba na baada ya awamu hii ili kupunguza hatari ya Kuvuja Damu baada ya Kuzaa. Vidokezo vilivyo muhimu vimeandikwa kwa muhtasari hapa.
- Ipapase uterasi (iwapo umehitimu kufanya hivyo) kwa kufinya kwa mikono miwili (Kipindi cha 11).
- Mpe mama kipimo cha pili cha oxytocin 10IU kwa kumdunga ndani ya misuli au umpe kipimo cha pili cha misoprostol 400 µg. Mpe misoprostol kupitia kwenye rektamu. Zisukume kwa utaratibu tembe hizi ndani ya rektamu kupitia kinyeoni cha mwanamke huyu, au uziweke chini ya ulimi wake ili ziyeyuke.
- Mhimize kuanza kunyonyesha punde baada ya kuzaa. Mikazo inayotoa maziwa hukazisha uterasi.
Usizidishe vipimo 1,000 µg za misoprostol (tembe 5). Iwapo mwanamke atatumia vipimo 600 µg (tembe 3) baada ya kuzaa na anavuja damu kwa wingi, usimpe zaidi ya 400 µg (tembe 2) kupitia rektamu Kipimo sahihi hakisababishi madhara. Iwapo hakutumia vipimo 600 µg vya misoprostol kupitia mdomoni baada ya kuzaa na anavuja damu kwa wingi, mpe vipimo 1,000 µg vya misoprostol kupitia rektamu kwa kipimo kimoja.
Iwapo oxytocin ilitumika mwanzoni, usimpe misoprostol zaidi.
Iwapo mwanamke huyu atavuja damu kwa wingi, mpeleke kwenye kituo cha afya mara moja. Kipindi cha 11 kitakufunza hatua za kuchukua wakati wa safari.
Iwapo damu haikomi kuvuja upesi baada ya kipimo cha pili cha misoprostol, mpendekezee rufaa ya dharura kwenda katika kituo cha afya kilicho karibu. Wakati mwingine, damu huvuja kutoka kwenye uke uliojeruhiwa, seviksi iliyojeruhiwa au uterasi iliyojeruhiwa. Kwa kawaida, damu hii huvuja kwa mchiririko wa polepole na usiokoma. Damu hii kwa kawaida huwa nyembamba na ya rangi nyekundu ng’avu. Hatua za kuchukua unaposubiri uchukuzi:
- Mlaze mama huku miguu yake ikiwa imeinuka kuzidi kichwa, na kichwa chenyewe kikiegemea upande mmoja. Mpashe joto kwa kumfunika blanketi.
- Ufunge vyema mpira wa kutilia viowevu kisha uanze kumtia kiowevu kwa kutumia kiowevu cha kawaida cha chumvi au Kiowevu cha Ringer. (Ulijifunza jinsi ya kuanza kuongeza kiowevu mwilini katika Kipindi cha 22 cha Moduli ya Utunzaji wa kabla ya kuzaa, na katika mafunzo yako ya kiutendaji.) Unaweza kufunzwa jinsi ya kuongeza kipimo kingine cha oxytocin katika viowevu vilivyo katika mfuko unaobebea mipira ya kuongeza viowevu mwilini. Hata hivyo, unaweza kumpa oxytocin iwapo tu unweza kuihifadhi ndani ya friji hadi utakapoihitaji.
- Dumisha usafi kwenye vulva na msamba.
- Ikwezekana, ambatana na mwanamke huyu hadi hospitalini.
- Wahimize jamaa au rafiki zake kuandamana naye na kumtunza mtoto (na kuwatolea damu ikihitajika).
6.2 Udhibiti tendeti katika hatua ya tatu ya leba (UTATL)