6.3.2 Plasenta iliyosalia
Plasenta iliyosalia ni wakati plasenta imesalia ndani ya uterasi kwa zaidi ya dakika 30 baada ya mtoto kuzaliwa. Iwapo plasenta itasalia ndani ya uterasi kwa zaidi ya dakika 30, fanya mambo yafuatayo:
- Usijaribu kuivuta zaidi kambakitovu ukitaka kuitenganisha na plasenta.
- Mtayarishe mwanamke huyu kusafirishwa hadi katika kituo cha afya kwa utunzaji wa dharura haraka iwezekanavyo. Fuata maagizo yaliyopeanwa katika kitengo kilichotangulia.
Back to previous pagePrevious
6.3 Usaidizi katika matatizo baada ya kutumia UTATL