Muhtasari wa Kipindi cha 6 cha Somo

Katika Kipindi cha 6, ulijifunza yafuatayo:

  1. Udhibiti tendeti katika hatua ya tatu ya leba (UTATL) ndio njia bora zaidi ya kupunguza hatari ya Kuvunja damu baada ya Kuzaa kwa zaidi ya 60%. Kwa hivyo, tumia UTATL kwa kina mama wote wanaozaa.
  2. Mabadiliko mtawalia ya kifisiolojia yanayofanyika katika awamu ya tatu ya leba ni: kutengana kwa plasenta, kushuka kwa plasenta, kutolewa kwa plasenta na kudhibiti kuvuja kwa damu.
  3. Matatizo ya kawaida yanayoweza kutokea katika awamu ya tatu ya leba ni pamoja na plasenta iliyosalia, kuvuja damu baada ya kuzaa na kugeuka kwa uterasi.
  4. Njia ya UTATL ina vipengele vifuatavyo mtawalia: Chunguza kama kuna mtoto mwingine, mpe mama dawa za ndani ya uterasi zinazoikazisha, na utumie njia ya kuvuta kambakitovu taratibu. Ipapase uterasi baada ya kutolewa kwa plasenta, ichunguze plasenta kuona kama ni nzima, na uchunguze sehemu ya uke kutambua kama kuna majeraha na damu inayovuja kwa wakati huu.
  5. Oxytocin, ergometrine namisoprostol ni dawa za kukazisha uterasi zinazotumika mara nyingi. Ergometrine ni dawa yenye nguvu sana, hivyo haipendekezwi kutumiwa katika Huduma ya Afya Ugani. Ni sharti Oxytocin na ergometrine zihifadhiwe ndani ya friji hadi zitakapohitajika. Misoprostol huwa ni tembe.
  6. Tumia misoprostol au oxytocin kabla ya muda usiozidi dakika moja baada ya kuzaliwa kwa mtoto.
  7. Hakikisha kuwa uterasi imekazana ifaavya hadi kuwa ngumu. Uterasi inaonekana ikiwa imejichora juu ya fumbatio. Hauoni damu inayovuja, isipokuwa unaona miraruko au majeraha kwenye sehemu ya chini ya uke.
  8. Ikihitajika, andaa mpira wa kuongeza viowevu mwilini na ujitayarisha kupendekeza rufaa hadi katika kituo cha afya. Pendekeza rufaa iwapo utaona mojawapo ya dalili hizi: ndewe ya plasenta ambayo haipatikani, plasenta iliyosalia na uterasi nyororo, legevu na iliyopanuka. Pendekeza rufaa iwapo utatambua damu inayoendelea kuvuja hata baada ya kurudia utaratibu wa kumpa mama dawa ya ndani ya uterasi na kuipapasa uterasi.

6.3.2 Plasenta iliyosalia

Maswali ya Kujitathmini ya Kipindi cha 6