Maswali ya Kujitathmini ya Kipindi cha 6

Kwa kuwa sasa umekamilisha kipindi hiki, jibu maswali yafuatayo ili kubaini jinsi ulivyojifunza. Unaweza kulinganisha majibu yako na uliyoandika kwenye Maswali ya Kujitathmini mwishoni mwa Moduli hii.

Swali la Kujitathmini 6.1 (linatathmini Malengo ya Somo la 6.1 na 6.2)

 • a.Fasili ya awamu ya tatu ya leba ni nini?
 • b.Ni mabadiliko gani ya kimwili yanayotokea katika awamu ya tatu ya leba ya kawaida isiyokuwa na matatizo?

Answer

 • a.Awamu ya tatu ya leba huanza kwa kuzaliwa kwa mtoto na kuisha kwa kutolewa kwa plasenta na membreni zilizoungana nayo.
 • b.Mabadiliko ya kimwili yafuatayo hutokea katika awamu ya tatu ya leba ya kawaida:
  • Plasenta inapobambuka kutoka pembezoni mwa uterasi, damu iliyo ndani ya vishipa vidogo kwenye mzizi wa plasenta huanza kugandia katikati mwa pembezoni mwa plasenta na miometriamu. (Miometriamu ni pembezo ya uterasi iliyoundwa kwa misuli.)
  • Plasenta hushukia chini ya njia ya uzazi hadi kupitia seviksi iliyopanuka. Baadaye, plasenta hutolewa.
  • Baada ya plasenta kutolewa, misuli ya uterasi hukazana. Misuli hii huifinya mishipa iliyopasuka ili kusitisha damu kuvuja baada ya kuzaa. Uterasi hugeuka kuwa ngumu na ya duara.

Mwisho wa jibu

Swali la Kujitathmini 6.2 (linatathmini Malengo ya Somo 6.1 na 6.3)

Alemitu ni Mhudumu wa Afya Ugani katika Kituo cha afya cha kijijini. Amemaliza kuzalisha katika kituo chake muda mfupi uliopita. Mama anayemhudumia yuko katika awamu ya tatu ya leba, na ameanza kunyonyesha. Alemitu amehitimu kutumia UTATL. Hatua 6 za UTATL, kwa kina, ni zipi?

Answer

Hatua 6 za UTATL ni kama ifuatavyo:

1: je, kuna mtoto wa pili?

2 Mpe mama dawa ya kukazisha uterasi ili kuiwezesha kukazana:

 • Tembe za misoprostol (mikrogramu) 600 μg zinazonywewa kwa maji.
 • Au umpe oxytocin 10 IU inayodungwa ndani ya misuli.
 • USIMPE ergometrine.

3 Itoe plasenta kwa kutumia njia ya kuvuta kitovu taratibu kwa msukumo pinzani (Kisanduku 6.3 kinaeleza kwa kina.)

4 Papasa uterasi

5 Ichunguze plasenta na membreni za fetasi kuhakikisha kuwa hakuna vipande vilivyosalia. Chunguza ndewe na sehemu ya juu ya mama. Tia mkono wako ndani ya membreni kuhakikisha kuwa membreni hizi ni nzima. Hakikisha kuwa hali ya kambakitovu ni ya kawaida.

6 Chunguza uke na sehemu ya nje ya uke wa mama ili kutambua kama kuna mchibuko au damu inayovuja.

Mwisho wa jibu

Swali la Kujitathmini 6.3 (linatathmini Malengo ya Somo 6.3)

Husika kwa Utendeti katika Kudhibiti Awamu ya Tatu ya Leba Ulitumia UTATL ifaavyo, lakini mwanamke huyu ameendelea kuvuja damu.

 • a.Je, utampa misoprostol zaidi? Kama ni hivyo, ni kipimo kipi cha dawa unachofaa kumpa, na dawa yenyewe inafaa kuwa katika aina gani?
 • b.Je, ni hatua ipi nyingine unayofaa kuchukua?
 • c.Unafaa kufanya nini iwapo mwanamke huyu ataendelea kuvuja damu?

Answer

 • a.Ndiyo, lakini usizidishe vipimo 1,000 µg za misoprostol kwa ujumla. Iwapo umeshampa vipimo 600 μg vya dawa, unaweza kumpa hadi vipimo 400 μg zaidi. Ili kumpa kipimo cha pili, zitie tembe hizi ndani ya rektamu ya mwanamke huyu.
 • b.Mama huyu ameshaanza kunyonyesha, hivyo ipapase uterasi yake kwa kusukuma kwa mikonno miwili ili kusisimua mikazo.
 • c.Iwapo damu haikomi kuvuja upesi baada ya kipimo cha pili cha misoprostol, mpendekezee rufaa ya dharura kwenda katika kituo cha afya kilicho karibu. Anza kumwongeza viowevu mwilini kabla ya kuondoka.

Mwisho wa jibu

Swali la Kujitathmini 6.4 (linatathmini Malengo ya Somo 6.6)

Je, dalili hatari zinazoashiria matatizo yanayoweza kutokea katika awamu ya tatu ya leba ni zipi?

Answer

Dalili hizi hatari ni ishara ya matatizo katika awamu ya tatu ya leba:

 • Plasenta iliyosalia au plasenta ambayo ni kipande kimoja tu kilichotolewa
 • Seviksi inayofungika kabla ya plasenta kutolewa
 • mikazo hafifu ya uterasi
 • Unapoipapasa uterasi, unatambua kuwa ni nyororo.
 • Awamu ya tatu ya leba inayodumu kwa dakika 30.
 • Kuchibuka kwa msamba, uke au seviksi
 • Kuvuja damu kwa wingi (kuvuja damu baada ya kuzaa)

Mwisho wa jibu

Muhtasari wa Kipindi cha 6 cha Somo