7.2 Aina za uhaishaji wa mtoto mchanga
Jifunze hizi aina tatu za uhaishaji wa mtoto mchanga.
Upitishaji wa hewa safi: Tumia mfuko wa ambu unaotumika kwa mkono (Picha 7.3). Iweke barakoa kwenye pua na mdomo wa mtoto na usukume hewa kwenye mapafu ya mtoto huyo. (Wakati mwingine wataalamu wa afya hutumia neno “uwekaji mfuko wa ambu” kumaanisha upitishaji wa hewa safi.)
- Ufyonzaji: Tumia sirinji ya balbu kuondoa kamasi na viowevu kwenye pua na kinywa cha mtoto.
- Usingaji wa moyo: Finya kifua cha mtoto kwa mkazo mkali na hafifu ili kuchochea mpigo wa moyo (Picha7.4).
Back to previous pagePrevious
7.1.2 Asifiksia ya mtoto mchanga