7.4.3 Shughuli za kwanza
Fanya shughuli hizi kwa watoto wote wachanga bila kuzingatia kiwango cha asifiksia:
- Kwa haraka mpanguze mtoto asiwe na viowevu juu ya mwili wake (Mchoro 7.7).
- Hakikisha mtoto ana joto.
- Ondoa vizuizi vyovyote kwenye mdomo na pua (Picha 7.9).
- Mpapase kwa upole ili kuchochea aanze kupumua au kumsaidia katika kupumua (Mchoro 7.10).
- Wakati huo huo, kadiria kiwango cha asifiksia (Majedwali 7.1 hadi 7.3).
- Mweke mtoto kwa nafasi bora tayari kwa uhaishaji ukiona dalili za asifiksia (Picha 7.11).
Chunguza kila picha kwa makini. Soma muhtasari na maelezo yazo.
Back to previous pagePrevious
7.4.2 Chunguza kiwango cha mpigo wa moyo wa mtoto mchanga