7.4.6 Mguse kwa upole ili kumchochea kuanza upumuaji au kumsaidia katika kupumua
Usimchochee kwa vitendo hivi.
Aina hizi za kuchochea ni hatari na zinaweza kumjeruhi mtoto huyu mchanga.
- Usimpige kofi mgongoni.
- Usimminye ngome ya mbavu.
- Usisukume mapaja ya mtoto kwenye fumbatio lake.
- Usitanue msuli (sfinkta) wa mkundu.
- Usitumie vishinikizo moto au baridi wala kumwogesha kwa maji moto au baridi.
- Usitingize kiungamwana.
Back to previous pagePrevious
7.4.5 Ondoa vizuizi kwenye kinywa na pua