7.4.7 Iwapo utatambua asifiksia, anza uhaishaji!
Mlalishe chali mtoto huyu mchanga huku shingo lake likiwa limenyooshwa kidogo jinsi ilivyoonyeshwa kwenye picha ya kwanza katika mchoro 7.11. Fyonza kinywa na pua kwa sirinji aina ya balbu. Kufyonza hufungua njia ya hewa (Picha 7.9).

- Simama upande wa kichwa cha mtoto (Mchoro 7.12).

Ikiwa mpigo wa moyo wa apeksi ni zaidi ya mipigo 60 kwa dakika:
- Pitisha hewa kwa barakoa yenye ukubwa ufaao na mfuko wa ambu unaopitisha hewa wenyewe. Barakoa inafaa kutosha jinsi ilivyoonyeshwa katika Mchoro 7.13. Tengeneza kizibo imara kati ya barakoa na uso wa mtoto ili hewa isipite kutoka kwa barakoa hiyo. Usilazimishe barakoa kwenye uso wa mtoto, kwani unaweza kusukuma kidevu kuelekea kwenye kifua cha mtoto na uishie kubana njia yake ya hewa. (Mchoro wa tatu katika Mchoro 7.11.)
Ikiwa mpigo wa moyo wa apeksi ni chini ya mipigo 60 kwa dakika:
- Usinge moyo (Mchoro 7.4) na upitishe hewa safi kwa kusita kwa mfuko wa ambu.

7.4.6 Mguse kwa upole ili kumchochea kuanza upumuaji au kumsaidia katika kupumua