Muhtasari wa Kipindi cha 7
Katika Kipindi cha 7, umejifunza mambo haya:
- Dalili za asifiksia kwa watoto wachanga wakati wa kuzaliwa ni: ugumu katika kupumua, kutweta, au kutopumua, mpigo wa moyo usio wa kawaida, udhaifu wa misuli (miguu na mikono dhaifu), kukosa kusonga, ngozi kuwa na rangi ya samawati (sinosisi) au kuchafuliwa na mekoniamu.
- Tathmini kiwango cha asifiskia katika sekunde 5 za kwanza baada ya mtoto kuzaliwa, wakati sawa na utakapoanza kutoa utunzaji wa kimsingi kwa mtoto mchanga. (Kwa mfano mpanguze mtoto, hakikisha anapata joto, kisha ufunge na ukate kiungamwana.)
- Kwa mtoto asiyepumua vizuri, fyonza mdomo na pua haraka na uanze kumhaisha.
- Chunguza kuhakikisha kuwa mtoto yuko hai. (Sikiliza mpigo wa apeksi wa moyo.) Chunguza kuhakikisha kuwa kiwango cha mpigo wa moyo ni zaidi ya mipigo 60 kwa dakika. (Ikiwa kiwango hiki ni chini ya mipigo 60 kwa dakika, usinge moyo kabla ya uhaisho.) Chunguza kuwa mtoto hajachafuliwa na mekoniamu. Fyonza uondoe mekoniamu kabla ya kumhaisha mtoto.
- Mweke mtoto katika hali ambapo shingo lake litanyooka ili kuzifungua njia za hewa. Mwekee barakoa ya kuingiza hewa safi inayotosha sawasawa juu ya mdomo na pua lake. Mpe hewa safi kwa kiwango cha pumzi 40 kwa dakika.
- Chunguza dalili zozote za nafuu: chunguza; rangi ya waridi, kusonga, na uwezo wa kupumua bila usaidizi. Usipoona nafuu baada ya dakika 30 za kumpa hewa safi, mpe rufaa haraka iwezekanavyo.
- Fanya shughuli zote za utunzaji muhimu kwa mtoto mchanga. Utunzaji kwa kiungamwili. Mdunge sindano ya vitamini K na lihamu ya macho ya tetrasaiklini. Anzisha kunyonyesha mapema na pasipo kumpa mtoto chakula kingine chochote. Hakikisha dawa za kuzuia VVU zimepeanwa ili kuzuia maambukizi kutoka kwa mama hadi kwa mtoto.
Back to previous pagePrevious
7.5 Utunzaji muhimu wa mara moja wa mtoto mchanga