8.1.3 Kutokuwa katika nafasi ya kawaida

Mtoto anaweza pia kuwa katika nafasi isiyo ya kawaida hata akiwa ametanguliza veteksi. Inaweza kuwa vigumu kugundua inapotendeka. Katika uzazi wa kawaida, wakati kichwa cha mtoto kimekabiliwa kwenye pelvisi, upande wa nyuma wa fuvu la kichwa cha mtoto huelekezwa upande wa mbele wa pelvisi ya mama. Upande wa nyuma wa fuvu la kichwa cha mtoto huitwa kisogo. Upande wa mbele ya pelvisi ya mama huitwa simfisisi ya kinena.Simfisisi ya kinena ni mahali ambapo mifupa miwili ya kinena inaungana pamoja. Hali hii ya fuvu la kichwa cha fetasi huitwa hali ya kisogo kuwa upande wa mbele (Picha 8.2a). Ikiwa kisogo cha fuvu la kichwa cha mtoto kinaelekea upande wa nyuma wa mama, hali hii ya kisogo kuwa upande wa nyuma (Picha 8.2b) ni veteksi kutokuwa katika nafasi ya kawaida. Ni vigumu zaidi kwa mtoto kuzaliwa akiwa katika hali hii. Uzuri ni kwamba zaidi ya takriban asilimia 90 ya watoto ambao veteksi haiko katika nafasi yake huzunguka na kuwa katika hali ya kisogo kuwa upande wa mbele na kuzaliwa kikawaida.

Ulijifunza nafasi za mwelekeo: mbele na nyuma katika Moduli ya Utunzaji katika Ujauzito, sehemu ya 1, Kipindi cha 3.

Tambua kwamba fuvu la kichwa cha mtoto pia linaweza kulazwa upande wa kushoto au wa kulia katika hali ya kisogo kuwa upande wa mbele au upande wa nyuma.

Picha 8.2 Hali zinazowezekana za fuvu la kichwa cha fetasi mtoto atangulizapo veteksi wakati mama amelala chali: (a) Hali ya kawaida “isiyopinda” ya kisogo kuwa upande wa mbele ambapo mtoto anaweza kuzaliwa kwa urahisi sana. (b) Hali ya kutokuwa katika nafasi ya kawaida na “isiyopinda” ya kisogo kuwa upande wa nyuma hufanya kuzaa kuwe na ugumu zaidi. (Imetolewa: Kwa heshima ya Mikael Häggström, imefikiwa kwenye http://commons.wikimedia.org/ wiki/ File:Cephalic_presentation_-_straight_occipito-anterior.png [Tip: hold Ctrl and click a link to open it in a new tab. (Hide tip)] )

8.2 Visababishi na athari za milalo mibaya na hali ya kutokuwa katika nafasi ya kawaida