8.4.1 Visababishi vya mlalo wa kutanguliza uso
Visababishi vya mlalo wa kutanguliza uso ni sawa na vile vya mlalo wa kutanguliza matako:
- Ulegevu wa uterasi baada ya ujauzito mwingi uliokomaa hapo awali
- mimba ya pacha
- Polihadromino (kiowevu cha amnioni kingi kupita kiasi)
- Matatizo ya kuzaliwa ya mtoto (kwa mfano anensefalia, yaani kukosekana au kutokua vizuri kwa mifupa ya fuvu la kichwa)
- Umbo lisilo la kawaida la pelvisi ya mama
Back to previous pagePrevious
8.4 Mlalo wa kutanguliza uso